Kuamka kwa hisia za mapenzi zinazopelekea kusimama kwa uume husababisha kuongezeka kwa mzunguko wa damu maeneo ya mfumo wa uzazi(uume na maeneo ya kinena. Kuongezeka kwa shinikizo hili la damu maeneo haya huweza kuambatana na maumivu kwa baadhi ya watu. Hata hivyo maumivu haya huisha mara moja baada ya kufika kileleni(kumwaga mbegu). Kuna baadhi ya visabababishi vinavyoweza kuwa vya hatari zaidi kama kujisokota kwa korodani au magonjwa ndani ya korodani ambayo yanahitaji matibabu ya haraka. Onana na daktari wako ili kujua ni nini tatizo kama una dalili hii.
Soma zaidi kuhusu maumivu ya korodani na visababishi vyake kwa kubonyeza hapa