Zipo njia nyingi unawezakuzitumia kukusaidia kupunguza uzito wako, njia hizo ni pamoja na;
Njia ya upasuaji
Chagua aina ya njia kusoma maelezo zaidi
Maelezo kwa ufupi kuhusu njia mbalimbali za kupunguza mwili(endapo utataka kusoma maelezo ya ziada bonyeza kichwa cha makala husika)
Haya ni mazoezi ambayo yatafanya mwili wako utumie nguvu nyingi unazozipata kutoka kwenye chakula, mazoezi haya yanapofanyika huweza kukusababishia kupata njaa zaidi na kula zaidi. Unashauriwa usiongeze kiasi cha chakula unachokula ili kuepuka kuongezeka mwili zaidi wakati wa mazoezi. Kuna aina kadhaa za mazoezi yanayoweza kufanyika ikiwa pamoja na mazoezi ya aerobiki, mazoezi ya anaerobiki, mazoezi ya ukinzani n.k. Bonyeza hapa kusoma zaidi
Njia hii hutumika kusafisha sumu mbalimbali mwilini, pia huwezesha mwili kubadilisha mfumo wake wa utafsiri wa kile unachokula. Mfumo huu unahusisha namna ubongo wako ulivyokuzoesha kupenda au kuchukia vyakula aina fulani, pia kukupa hamu ya kula vyakula hivyo kwa wingi. Mbali na hivyo pia njia hii hufanya mwili wako uondoe sumu ambazo zimekusanyika mwilini mwako zinazoharibu mfumo wa asilia wa ubongo dhidi ya utafsiri kuhusu chakula unachokula. Soma zaidi makala hii kwa kubonyeza hapa.
NJia hii imekuwa ikitumika sana kwa karne hii, kuna mafundisho mengi yanayohusu vyakula na kupunguza uzito. Baadhi ya mafundisho huelekeza uache kabisa kula vyakula vyenye wanga, baadhi hutaka upunguze vyakula vya wanga na kuongeza matunda kwa wingi na mboga za majani. ULY CLINIC inashauri njia hii inaweza kutumika kwa uangalizi wa kuhakikisha kuwa haukosi virutubisho muhimu kutoka kwenye chakula. Madhara ya kutumia njia hii ni kwamba mara baad aya kuacha kuzingatia chakula uzito utarejea mara dufu zaidi ya awali kama adhabu ya mwili dhidi ya kipindi chote ulichopunguza uzito. Habari njema ni kwamba njia hii huweza kukusababisha upungue uzito kwa haraka zaidi kuliko njia nyingine. bonyeza hapa kusoma zaidi
Dawa nyingi za kupunguza uzito hufanya kazi katika misingi ya kupunguza ufyonzwaji wa chakula unachokula, kupunguza hamu ya kula na kupunguza umetabolizi wa sukari kwenye damu. Njia ya dawa imegawanyika kwenye makundi mawili ambayo ni dawa asilia na kundi la pili ni dawa za hospitali ambazo utaandikiwa na daktari wako.Kuna matokeo mazuri sana endapo mtu atatumia njia ya dawa pamoja na mazoezi na kuzingatia chakula. Bonyeza hapa kusoma zaidi
Hii ni njia ambayo watu wengi kwa afrika bado hawaijui, njia hii inatumika kuondoa mafuta yaliyozidi kwa kuyayeyusha au kuyakata na kisu maalumu katika chumba cha upasuaji. Njia hii hufaa zaidi kwa watu wenye unene zaidi na nyama uzembe, huwa na matokeo mazuri na ya haraka. Uzito wa mtu unaweza kujirudia endapo mtu hatazingatia chakula lakini huchukua muda mrefu kiasi. Soma zaidi kuhusu makala hii kwa kubonyeza hapa
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na mtaalamu wako wa afya baada ya kusoma makala hii, kabla ya kuchukua hatua yoyote ile dhidi yako. Daktari wako atapangia namna ya kupunguza uzito kulingana na mahitaji ya mwili wako bila kupata madhara makubwa.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa maswali zaidi, ushauri na Tiba dhidi ya uzito mkubwa kwa kubonyeza hapa au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.