Kiafya unaposema nyama nyeupe tunamaanisha nyama yenye rangi iliyopauka. Nyama iliyopauka huwa na kiasi kidogo cha mayoglobin ambayo ni protini maalumu inayobeba oksijeni kwa matumizi ya misuli na pia huipa misuli rangi yake nyekundu. Nyama nyeupe hupatikana sana kwenye viumbe jamii ya ndege haswa kwenye nyama ya kifua. Baadhi ya sehemu za viumbe ndege zinazofanya kazi sana ya kuwezehsa ndege kupaa au kukimbia huwa na kiwango kingi cha mayoglobin huvyo huonekana kuwa na rangi nyekundu. Nyama ya miguu na mabawa ya wanyama jamii ya ndege kama kuku licha ya kuwa na rangi nyekundu, huwa na kiwango kidogo cha mayoglobin ukilinganisha na nyama ya wanyama.
Viumbe gani waana nyama nyeupe
Viumbe vifuatavyo huwa na nyama nyeupe;
Bata maji
Kuku
Bata mzinga
Sungura
Samaki
Nyama nyeupe inafaida gani mwilini?
Kiwango cha kidogo cha madini chuma ya himu na mafuta yasiyoshamiri yanayopatikana kweye nyama nyeupe hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kutokana na kuziba kwa mishipa.
Hata hivyo nyama nyeupe ambazo zimehifadhiwa, huwa na kiwango kikubwa cha madini chumvi (sodiamu) ambacho hulinda nyama kuharibika. Chumvi hii huongeza hatari kubwa ya kupata shinikizo la juu la damu.
Wataalamu wanashauri kutumia nyama nyeupe ya viumbe ambao hawajahifadhiwa kabla ya kupika, yaani kama ni kuku awe ametoka kuchinjwa na kama ni samaki asiwe ameongezewa chochote cha kumfanya asiharibike. Kama ukiweza nunua viumbe hao wakiwa hai na kuwandaa mwenyewe.
Mbali na faida hizo,nyama nyeupe pia huwa na virutubisho na nishati muhimu kama ilivyoorodheshwa hapa chini
Nishati
Mafuta
Mafuta yaliyoshamiri
Protini
Madini ya fosforazi
Ingawa virutubisho vingine unaweza kuvipata kutoka kwenye vyakula vya mimea na nafaka, nyama, samaki na maziwa ni chanzo pekee cha vitamin B12 ambacho huwezi kukipata kutoka kwenye vyakula vya mimea
Utofauti kati ya nyama nyeupe na nyama nyekundu
soma kwa umakini kwa kufananisha nyama nyeupe na nyama nyekundu utaona utofauti wake kwenye virutubisho na nishati.
Gramu 100 za nyama ya kuku aliyetolewa mafuta (ngozi) huwa na;
Kilokalori 109 za Nishati
Gramu 0.43 za Mafuta
Gramu 1.28 za Mafuta yaliyoshamiri
Gramu 25.95 za Protini
Miligramu 207 za Madini fosforazi
Vilivyomo kwenye gramu 100 ya nyama nyekundi iliyoyolewa mafuta ni;
Kilokalori 123 za Nishati
Gramu 4.3 za Mafuta
Gramu 1.9 za Mafuta yaliyoshamiri
Gramu 21 za Protini
Miligramu 1.3 za Madini chuma
Miligramu 1.7 za Madini zinki
Miligramu 230 za Madini fosforazi
Miligramu 167 za Madini potasiamu
Miligramu 59 za Madini sodiamu
Baadhi ya maswali na majibu yanahusu nyma nyeupe
Nguruwe ni nyama nyeupe?
Hapana!
Nguruwe si nyama nyeupe, hata hivyo ukilinganisha na viumbe wengine wenye nyama nyekundu, nyama ya nguruwe huwa na kiasi kidogo cha mayoglobin.
Rejea za mada hii
White meat. https://www.oxfordreference.com/view/10.1093/oi/authority.20110803122317351. Imechukuliwa 04.07.2021
White vs. dark meat. https://www.chicken.ca/chicken-school/white-meat-vs-dark-meat-the-great-debate/. Imechukuliwa 04.07.2021
Beef nutritional facts. https://www.healthline.com/nutrition/foods/beef#nutrition. Imechukuliwa 04.07.2021
Nutritional composition of meat. https://www.intechopen.com/books/meat-science-and-nutrition/nutritional-composition-of-meat.
Beaf and fitness today. http://www.dietandfitnesstoday.com/phosphorus-in-beef.php. Imechukuliwa 04.07.2021
Monounsaturated Fat. https://www.heart.org/en/healthy-living/healthy-eating/eat-smart/fats/monounsaturated-fats. Imechukuliwa 05.07.2021
NCBI. CANCER IN HUMANS. General issues regarding the epidemiology of cancer and consumption of red meat and processed meat. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK507972/#:~:text=(a)%20Red%20meat,and%20is%20usually%20consumed%20cooked.imechukuliwa 17.07.2021