
Omeprazole ni moja ya dawa katika kundi la vizua pampu ya protoni (PPI) inayofanya kazi kwa kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni. Kwa kuzuia uzalishaji wa tindikali huweza kutibu magonjwa ya tumbo yanayosababishwa na uzalishaji mwingi wa tindikali.
Makala hii imezungumzia kuhusu magonjwa inayotibu, maudhi, madhara, na vizuizi vya matumizi ya Omeprazole.
Magonjwa yanayotibika kwa Omeprazole
Hali na magonjwa yafuatayo hutibiwa kwa kutumia omeprazole;
Kucheua tindikali- Huzuia uzalishaji wa tindikali
Vidonda vya tumbo- Huponya na kuzuia kufanyika kwa vidonda
Maambukizi ya Helicobacter pylori – Hutumika pamoja na antibiotiki kuua bakteria hawa.
Sindromu ya Zollinger-Ellison – Huzuia uzalishaji mwingi wa asidi tumboni.
Kuungua kwa Umio- Inasaidia uponyaji wa uharibifu wa umio unaosababishwa na asidi.
Vidonda vinavyosababishwa na matumizi ya dawa jamii ya NSAIDs – Huzuia vidonda kwa watumiaji wa muda mrefu wa dawa za maumivu jamii ya NSAIDs.
Maudhi ya Omeprazole
Yafuatayo ni maudhi ya matumizi ya dawa omeprazole;
Maumivu ya kichwa
Kichefuchefu, kutapika
Kuharisha au kukosa choo
Maumivu ya tumbo
Tumbo kujaa gesi
Kizunguzungu
Madhara ya omeprazole
Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea kwa watumiaji wa omeprazole;
Upungufu wa Vitamini B12 – Hupunguza ufyonzwaji wa vitamini B12 mwilini haswa kwa watumiaji wa muda mrefu.
Udhaifu wa mifupa na kuvunjika mifupa – Huongeza hatari ya mifupa kuwa dhaifu
Matatizo ya figo – Inaweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo.
Maambukizi ya Clostridium difficile – Inaweza kuongeza hatari ya kuhara kali.
Uzalishaji shamiri wa tindikali tumboni- Asidi ya tumbo huzalishwa kwa wingi baada ya kuacha dawa ghafla.
Watu wasiopaswa kutumia omeprazole
Hali na mambo yafuatayo huzuia watu kutumia au kuchukua tahadhari kabla ya kutumia ili kuepuka madhara;
Watu wenye mzio wa Omeprazole au dawa za PPI – Inaweza kusababisha athari kali za mzio.
Watu wenye magonjwa ya ini – Inaweza kuathiri utendaji wa ini.
Watu wenye upungufu wa magnesiamu – Matumizi ya muda mrefu yanaweza kupunguza kiwango cha magnesiamu.
Watu wenye ugonjwa wa mifupa dhaifu– Inapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwa wenye mifupa dhaifu.
Kuwa mjamzito au kunyonyesha – Inapaswa kutumiwa tu ikiwa ni lazima na kwa ushauri wa daktari.
Rejea za mada hii
Bium AL. Omeprazole: implications for therapy of peptic ulcer and reflux oesophagitis. Digestion. 1989;44 Suppl 1:87-91.
Laine L, et al. Twice-daily, 10-day triple therapy with omeprazole, amoxicillin, and clarithromycin for Helicobacter pylori eradication in duodenal ulcer disease: results of three multicenter, double-blind, United States trials. Am J Gastroenterol. 1998 Nov;93(11):2106-12.
Prasertpetmanee S, et al. Improved efficacy of proton pump inhibitor - amoxicillin - clarithromycin triple therapy for Helicobacter pylori eradication in low clarithromycin resistance areas or for tailored therapy. Helicobacter. 2013 Aug;18(4):270-3.
Bianchi Porro G, et al. Short-term treatment of refractory reflux esophagitis with different doses of omeprazole or ranitidine. J Clin Gastroenterol. 1992 Oct;15(3):192-8.
Sontag SJ, et al. Two doses of omeprazole versus placebo in symptomatic erosive esophagitis: the U.S. Multicenter Study. Gastroenterology. 1992 Jan;102(1):109-18.
Meijer JL,et al. Omeprazole in the treatment of Zollinger-Ellison syndrome and histamine H2-antagonist refractory ulcers. Digestion. 1989;44 Suppl 1:31-9.
Cooper BT, et al. Continuous treatment with omeprazole 20 mg daily for up to 6 years in Barrett's oesophagus. Aliment Pharmacol Ther. 1998 Sep;12(9):893-7.
Levy MJ, Seelig CB, Robinson NJ, Ranney JE. Comparison of omeprazole and ranitidine for stress ulcer prophylaxis. Dig Dis Sci. 1997 Jun;42(6):1255-9.
Sachs G, Wallmark B. The gastric H+,K+-ATPase: the site of action of omeprazole. Scand J Gastroenterol Suppl. 1989;166:3-11.
Howden CW. Clinical pharmacology of omeprazole. Clin Pharmacokinet. 1991 Jan;20(1):38-49.
Oosterhuis B, Jonkman JH. Omeprazole: pharmacology, pharmacokinetics and interactions. Digestion. 1989;44 Suppl 1:9-17.