
Penadur ni jina la kibiashara la dawa Benzathine Penicillin G, ambayo ni antibiotiki iliyogunduliwa miaka mingi iliyopita na na imekuwa ikitumika kwenye matibabu ya maambukizi ya bakteria.
Dawa hii hutumiwa kwa kuchoma sindano kwenye misuli katika matibabu ya magonjwa yanayosababishwa na bakteria wanaodhuriwa na dawa, sambamba na kutumika kama kinga ya homa ya baridi yabisi na maambukizi ya streptococcus kooni.
Magonjwa yanayotibika na Penadur injection
Kama maelezo ya awali, penadur injection hutibu maambukizi ya Streptococcus ambayo hutokea kwenye ko, ngozi na sehemu nyingine ya mwili mathalani;
Hutumika kama kinga ya homa ya baridi yabisi na ugonjwa wa moyo wa baridi yabisi
Hutibu kaswende na maambukizi mengine anayosababisha kimelea Treponema
Hutibu magonjwa ya ngozi kama Yaws, Bejel, na Pinta
Hutumika kama kinga dhidi ya bakteria kwenye figo kama kutokana na bakteria Streptococcus
Maudhi ya penadur injection
Baadhi ya maudhi ya kawaida ya penadur injection yanayotokea sana huwa kama yafuatayo;
Maumivu au uvimbe kwenye sehemu ilipochomwa sindano
Homa au kuhisi baridi
Kichefuchefu na kutapika
Upele wa ngozi mdogo
Madhara ya penadur injection
Baadhi ya maudhi makubwa au madhara ya penadur injection ni pamoja na;
Mzio Mkali unaoambatana na dalili za kupumua kwa shida, kuvimba uso, midomo, au koo
Sindromu ya Stevens-Johnson ambapo ni mwitikio mkali unaosababisha ngozi kupata malengelenge makubwa.
Mwitikio wa kinga wa Jarisch-Herxheimer wakati wa matibabu ya Kaswende – Dalili za mafua kutokana na bakteria kufa ghafla
Madhara ya mfumo wa neva ikiwa imeingizwa kimakosa kwenye mshipa wa damu (degedege, kuchanganyikiwa)
Watu wasiopasa kutumia penadur injection
Watu wafuatao wanapaswa kutotumia penadur injection kuepuka madhara isipokuwa endapo wameshauriwa na daktari;
Wanaosumbuliwa na mzio na dawa jamii ya Penicillin au Cephalosporins
Wenye pumu kali au historia ya mzio mkali
Wajawazito (matumizi tu kwa ushauri wa daktari)
Wenye ugonjwa wa figo (huenda wakahitaji marekebisho ya dozi)
Rejea za mada hii
Walker GJ,et al. Antibiotic treatment for newborns with congenital syphilis. Cochrane Database Syst Rev. 2019 Feb 15;2(2):CD012071.
Ndeikoundam Ngangro N, et al, referents for the regional offices of the French national public health agency. Pillonel J, Lot F. Bacterial sexually transmitted infections in France: recent trends and patients' characteristics in 2016. Euro Surveill. 2019 Jan;24(5)
Webber BJ, et al. Chemoprophylaxis against group A streptococcus during military training. Prev Med. 2019 Jan;118:142-149.
Struyve M, et al. Primary syphilitic proctitis : case report and literature review. Acta Gastroenterol Belg. 2018 Jul-Sep;81(3):430-432.
Khan A, et al. An old disease re-emerging: acute rheumatic fever. Clin Med (Lond). 2018 Oct;18(5):400-402.
Gozdas HT, Dogan A. Is Benzathine Penicillin the Treatment of Choice in Neurosyphilis? Am J Med. 2023 Oct;136(10):e208.
Dündaröz R, et al. Evaluation of DNA damage using the comet assay in children on long-term benzathine penicillin for secondary prophylaxis of rheumatic fever. Pediatr Int. 2001 Jun;43(3):276-80.
Kingston M, Carlin E. Treatment of sexually transmitted infections with single-dose therapy: a double-edged sword. Drugs. 2002;62(6):871-8.
Benzaken AS, et al. Adequacy of prenatal care, diagnosis and treatment of syphilis in pregnancy: a study with open data from Brazilian state capitals. Cad Saude Publica. 2019;36(1):e00057219.