Baada ya kujifungua, ni kawaida kwa mwanamke kutokwa na uchafu ukeni ambao huwa ni mchanganyiko wa ute wa kizazi, damu na masalia ya uzao wa mtoto na kondo la nyuma. Uchafu huu hubadilika rangi na harufu kwa jinsi kiasi cha damu kinavyopungua.

Kwa kawaida inachukua wastani wa siku 14 kwa uchafu kuisha, hata hivyo baadhi ya wanawawe inaweza kuchukua mpaka siku 21 na kuendelea. Mabadiliko ya rangi huanza kuwa nyekundu, kahawia, njano na baadae huwa na rangi ya ute wa kawaida.
Ratiba ya mabadiliko ya rangi ya uchafu
Uchafu ukeni hupitia hatua zifuatazo za mabadiliko ya rangi
Mabadiliko ya rangi: Kuanza nyekundu hudumu kwa siku 1 hadi 4
Rangi ya kahawia hudumu kwa kuda wa siku 5 hadi 9
Rangi ya njano inayodumu kuanzia siku ya 10 hadi 15
Wakati gani uwe na wasiwasi
Licha ya kutokwa na uchafu ukeni kuwa ni hali ya kawaida baada ya kujifungua, uonapo dalili zifuatazo unapaswa kupata ushauri wa daktari:
Homa
Uchafu kuwa na rangi ya kijani
Uchafu ukizidi wiki sita( siku 42)
Kuwa na harufu muozo
Maumivu makali ya tumbo la chini
Kizunguzungu
Mapigo ya moyo kwenda mbio
Rangi ya uchafu kuendelea kuwa nyekundu
Kuwa na mabonge kwa zaidi ya siku 3 za mwanzo
Kuhisi kitu kinatoka ukeni
Ute kuwa mwingi pasipo kupungua kwa jinsi siku zinavyoenda
Rejea za makala hii
Science direct. Lochia. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/lochia. Imechukuliwa 18.11.2024
NHS. Your body after the birth. https://www.nhs.uk/pregnancy/labour-and-birth/after-the-birth/your-body/. Imechukuliwa 18.11.2024
Postpartum Bleeding (Lochia): What's Normal and What's Not?https://www.whattoexpect.com/pregnancy/symptoms-and-solutions/postpartum-bleeding.aspx. Imechukuliwa 18.11.2024
Romano M, et al. Postpartum period: three distinct but continuous phases. J Prenat Med. 2010 Apr;4(2):22-5. Sherman D, Lurie S, Frenkel E, Kurzweil Y, Bukovsky I, Arieli S. Characteristics of normal lochia. Am J Perinatol. 1999;16(8):399-402.
Oppenheimer LW, et al. The duration of lochia. Br J Obstet Gynaecol. 1986 Jul;93(7):754-7.
Chi C, et al. Puerperal loss (lochia) in women with or without inherited bleeding disorders. Am J Obstet Gynecol. 2010 Jul;203(1):56.e1-5.