Swali:
Ugonjwa wa ngono unatibika adi kuisha?
Ugonjwa wa gono huwa unajirudia rudia?
Jibu:
Kama ugonjwa wa gono ukitibiwa kwa dawa na dozi sahihi na kwa kufuata maelekezo ya daktari, hutibika.
Wakati gani gono hujirudia?
Gono inaweza kujirudia endapo utashiriki mapenzi na mpenzi mwenye gono bila kutumia kinga. Ikumbumwe pia kama umepata gono na una mpenzi, anapaswa kutibiwa pia ili kuvunja mnyororo wa maambukizi. Endapo utatibiwa pekeyako na kupona, utakaposhiriki naye bila kinga ni lazima utapata maambukizi mengine.
Kuvunja mnyororo wa maambukizi
Kama mpenzi wako ana mpenzi mwingine, anapaswa kutibiwa, la sivyo maambukizi yataendelea kujirudia rudia.
Ili kuepuka maambukizi unashauriwa kufanga yafuatayo;
Kuwa na mpenzi mwaminifu asiye na maambukizi
Kutumia kinga endapo umepata mpenzi mpya au
Kufanya vipimo vya magonjwa ya zinaa kabla hujashiriki naye tendo
Kwa maelezo zaidi soma makala ya gono kwa wanawake au wanaume katika tovuti hii ya ulyclinic