Swali:
Ninatatizo la kwenda haja ndogo kila Mara wakati wa usiku lakini kwa mchana sio sana, huwa nashuku naeza kuwa na mimba ya karibu mwezi moja, inaeza kuwa ujauzito ndo husababisha?
Jibu:
Jibu linaweza kuwa Ndio au Hapana
Mojawapo ya dalili ya awali ya ujauzito ni kukojoa mara kwa mara, dalili hii huweza ambatana na dalili zingine zifuatazo;
Kuvimba matiti
Maumivu ya matiti
Kichefuchefu
Kichefuchefu na kutapika
Uchovu
Kupenda kula aina fulani ya chakula
Kupendelea sana kula aina fulani ya chakula
Kiunguli
Haja kubwa kuwa ngumu
Muda wa kukojoa sana
Kati ya wanawake 100, wanawake zaidi ya 80 wameripoti kukojoa sana wakati wa usiku wakati idadi ni hupatwa na dalili hii baada ya kucha.
Ikiwa una ujauzito, utapatwa mchanganyiko wa dalili hizo zinazoweza kutokea na kuondoka.
Wakati gani kukojoa mara kwa mara huashiria dalili isiyo ya kawaida?
Endapo unapata dalili ya kukojoa mara kwa mara inayoambatana na dalili zifuatazo inaweza kuwa si dalili ya inayosababishwa na ujauzito bali inaweza kusababishwa na maambukizi kwenye njia ya mkojo.
Maumivu wakati wa kukojoa
Kukojoa kwa shida au kushindwa kutoa mkojo
Maumivu ya tumbo
Homa
Kukojoa mkojo mzito au wenye mawingu
Ukipatwa na dalili hii unapaswa kufika kituo cha afya karibu nawe kwa uchunguzi na tiba.
Rejea za mada hii:
Adaji SE, et al. Bothersome lower urinary symptoms during pregnancy: a preliminary study using the International Consultation on Incontinence Questionnaire. Afr Health Sci. 2011 Aug;11 Suppl 1(Suppl 1):S46-52. doi: 10.4314/ahs.v11i3.70070. PMID: 22135644; PMCID: PMC3220122.
Aslan D, et al. Voiding symptoms in pregnancy: an assessment with international prostate symptom score. Gynecol Obstet Invest. 2003;55:46–49. [PubMed]
Chaliha C and Stanton S. Urological problems in pregnancy. BJU Int. 2001;89:469–476. [PubMed]
Fitzgerald MP and Graziano S. Anatomical and functional changes of the lower urinary tract during pregnancy. Urologic Clinics of North America. 2007;34:7–12. [PubMed]
Malpas P and Jeffcoate TNA, Lister UM. Displacement of the bladder and urethra in late pregnancy. J Obstet Br Emp. 1949;56:949–960. [PubMed]
Mikhail MS and Anyaegbunam A. Lower urinary tract dysfunction in pregnancy: a review. Obstet Gynecol Surv. 1995;50:675–683. [PubMed]
Sun MJ, et al. Prevalence of lower urinary tract symptoms during pregnancy in Taiwan. J Formos Med Assoc. 2005;104:185–189. [PubMed]
Thorp JM, et al. urinary incontinence in pregnancy and the puerperium: a prospective study. Am J Obstet Gynaecol. 1999;181:266–273. [PubMed]