Ulimi uliopasuka na kuwa na mifereji (ulimi kuchanika) ni tatizo linalojulikana sana, tatizo hili hutokana na matatizo asili ya kiuumbaji na hakuna kisababishi kinachofahamika kusababisha tatizo hili. Hata hivyo tatizo hili si saratani wala halina hatari ya kuwa saratani.
Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kwamba, ulimi uliopasuka na kuwa na mifereji Pamoja na tatizo la ulimi jiografia hurithiwa na huweza kuambatana pia na tatizo la soriasisi.
Mwathirika wa ulimi uliopasuka, ulimi wake huwa na mifereji mingi sehemu ya juu ya ulimi na kuwa na mwonekano jinsi Ngozi ya pumbu ilivyo. Mipasuko inaweza kutofautiana kwa upana,kina na idadi kutoka mtu mmoja na mwingine na mara nyingi huwa na mpangilio maalumu. Tatizo hili huwa halina dalili yoyote, hata hivyo uchafu wa chakula, vimelea na fangasi wanaweza kukaa kwenye kina cha mipasuko hii na kuleta uchokozi wkenye uimi na mtu kupata dalili za maumivu ya ulimi au kubadilika kwa ulimi.
Soma zaidi makala hii kwa undani kwa kubonyeza hapa
Soma kuhusu ulimi jiografia, ulimi kuuma na ulimi kuwaka moto bonyeza hapa