Uvumbuzi wa makundi ya damu kwa mfumo wa ABO uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliyopita ulileta furaha kwa wanasayansi Duniani kwa sababu ulisaidia kukabiliana na tatizo kubwa la madhara yaluiyokuwa yanatokea kwa kuongezewa damu isiyo sahihi kwa fikra kwamba damu za watu zinafanana.
Uvumbuzi huo ulianzisha safari nyingine ya kuelewa kuwa kundi la damu hurithiwa kizazi hadi kizazi na kundi la damu la mtoto anayezaliwa hutegemea makundi ya damu ya wazazi wake.
Makala hii imeeleza kuhusu urithishaji wa makundi ya damu kwa watoto kwa kuzingatia makundi ya damu ya wazazi.
Â
Aina ya makundi ya damu
Kuna makundi makuu 4 ya damu ambayo ni A, B, AB, na O. Watu wenye kundi O la damu hawana antijeni A wala B licha ya kuwa na afya njema.
Mwaka 1910 iligundulika kuwa makundi haya yad amu hurithiwa, na kundi A na B antijeni hutawala katika urithi.
Urithishaji wa makundi ya damu ni kama yalivyoelezewa kwenye jedwali na 1 hapa chini
Jedwali na 1: Ulithishaji wa kundi la damu kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto
Maelezo ya ziada ya jedwali namba 1
Endapo baba ni kundi A, na mama ni Kundi A, mtoto atakayezaliwa huwa na damu kundi A
Endapo baba ni kundi A na mama ni kundi B, Mtoto atakayezaliwa huwa kundi AB
Endapo baba ni kundi A na mama ni kundi O, mtoto atayezaliwa huwa ni kundi A
Endapo baba ni kundi B, na mama ni Kundi A, mtoto atakayezaliwa huwa na damu kundi AB
Endapo baba ni kundi B na mama ni kundi B, Mtoto atakayezaliwa huwa kundi B
Endapo baba ni kundi B na mama ni kundi O, mtoto atayezaliwa huwa ni kundi B
Endapo baba ni kundi O, na mama ni Kundi A, mtoto atakayezaliwa huwa na damu kundi A
Endapo baba ni kundi O na mama ni kundi B, Mtoto atakayezaliwa huwa kundi B
Endapo baba ni kundi O na mama ni kundi O, mtoto atayezaliwa huwa ni kundi O
Rejea za mada hii
Reid ME et al. The Blood Group Antigen Facts Book. Second ed. 2004, New York: Elsevier Academic Press.
Daniels G. Human Blood Groups, Second ed. 2002, Blackwell Science.
Stayboldt C , Rearden A , Lane TA . B antigen acquired by normal A1 red cells exposed to a patient's serum. Transfusion. 1987;27:41–4.
Reid ME , et al. Associations between human red cell blood group antigens and disease. Transfus Med Rev. 1990;4:47–55.
O'Donnell J , et al. The relationship between ABO histo-blood group, factor VIII and von Willebrand factor. Transfus Med. 2001;11(4):343–51.
Fuchs CS , et al . Gastric carcinoma. N Engl J Med. 1995;333:32–41.
Sazama K . Reports of 355 transfusion-associated deaths: 1976 through 1985. Transfusion. 1990;30:583–90.