Usubi ni ugonjwa unaofahamika pia kama Onchocerciasis(onkosekiasisi).
Utangulizi
Usubi ni maambukizi yanayosababishwa na mdudu mwenye vimelea wa Onchocerca volvulus, anayeenezwa kwa kuumwa na inzi mweusi aliyeambukizwa jamii ya Simulium. Pia huitwa upofu wa mtoni kwa sababu nzi anayesambaza maambukizi huzaliana katika vijito vinavyotiririka maji kwa kasi, hasa karibu mashamba ya vijijini, na ugonjwa waupofu unaosababishwa na O. volvulus kufuatia kuumwa mara kwa mara na inzi hao.
Watu walio na maambukizi mazito huwa na hali moja au zaidi kati ya hizi tatu, upele wa ngozi (mara nyingi huwasha), ugonjwa wa macho, au vinundu chini ya ngozi. Utafiti wa Global Burden of Disease Study ulikadiria kuwa mwaka 2017 kulikuwa na angalau watu milioni 20.9 walioambukizwa duniani kote, kati yao milioni 14.6 walikuwa na ugonjwa wa ngozi na milioni 1.15 walikuwa na upotevu wa kuona. Zaidi ya asilimia 99 ya watu walioambukizwa wanaishi Afrika; waliobaki wanaishi huko Yemen na Amerika ya Kusini.
Je, Usubi hueneaje?
Ugonjwa huu huenea kwa kuumwa na inzi mweusi aliyeambukizwa. Nzi mweusi anapomuuma mtu aliye na Usubi, mabuu ya minyoo midogo isiyoonekana kwa macho (inayoitwa microfilariae) kwenye ngozi ya mtu aliyeambukizwa humezwa na inzi mweusi. Vibuu hukua kwa takriban wiki moja katika inzi hadi hatua ambayo ni ya kuambukiza kwa binadamu. Inzi mweusi anayeambukiza kwa kawaida hudondosha mabuu anapomuuma mtu. Kisha mabuu hupenya kwenye ngozi ili kumwambukiza mtu. Kwa sababu minyoo huzaliana ndani ya binadamu pekee na kukamilisha baadhi ya hatua za ukuaji wao ndani ya inzi mweusi, nguvu ya maambukizi kwa binadamu (idadi ya minyoo kwa mtu mmoja mmoja) inategemea idadi ya kuumwa na mbu. Upofu kwa kawaida huonekana katika mazingira ya maambukizi ya muda mrefu na makali.
Ni nani aliye katika hatari zaidi ya kuoata usubi?
Walio hatarini zaidi ni watu wanaoishi au kufanya kazi karibu na vijito au mito inayotiririka maji kwa kasi ambapo kuna inzi weusi wa Simulium, wakifuatwa na wamishonari wa muda mrefu, wajitoleaji wa Peace Corps, watafiti wa nyanjani, na wasafiri wengine wa muda mrefu ambao wako katika hatari zaidi ya kuumwa mara nyingi na inzi weusi walioambukizwa na vimelea. Ugonjwa huu huenezwa sana katika vijiji vya kilimo vya pembezoni vya Kiafrika ambavyo viko karibu na vijito na mito inayotiririka kwa kasi.
Maeneo mengi ambayo inzi weusi hupatikana ni maeneo ya mashamba ya kilimo katika Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara katika nchi zilizotajwa hapo awali. Kawaida, kuumwa mara nyingi huhitajika kabla ya kuambukizwa ugonjwa.
Dalili
Watu walioambukizwa wanaweza wasionyeshe dalili. Wale walio na dalili huwa na dalili moja au zaidi kati ya hizi tatu:
Upele wa ngozi (mara nyingi huwashwa)
Ugonjwa wa macho
Vinundu chini ya ngozi
Dalili kali zaidi na mbaya ni vidonda kwenye jicho ambavyo vinaweza kusababisha uharibifu wa jicho hivyo kupelekea upofu.
Ni siku ngapi baada ya kuambukizwa nitapata dalili za usubi?
Baada ya kung'atwa na inzi mweusi, inaweza kuchukua hadi miezi 12-18 kwa mabuu kukua na kuwa minyoo waliokomaa ndani ya mwili wa binadamu ambao wana uwezo wa kujamiiana na kutoa mabuu wapya (pia huitwa microfilariae) ambao wanaweza kupatikana kwenye ngozi. Kila mdudu jike aliyekomaa, ambaye anaweza kuishi takriban miaka 10-15, anaweza kutoa mamilioni ya mabuu wapya katika maisha yake. Kwa vile ni mabuu ambayo husababisha dalili za Usubi, watu wengi walioambukizwa na O. volvulus huwa hawapati dalili yoyote hadi baada ya minyoo waliokomaa kuanza kuzalisha idadi kubwa ya mabuu wapya.
Nifanye nini ikiwa nadhani ninaweza kuwa na usubi?
Ikiwa unafikiri unaweza kuwa na usubi, onana na mtoa huduma wako wa afya ambaye anaweza kuagiza kipimo cha kinyama cha ngozi (biopsies) au vipimo vya damu kutafuta kingamwili kwa vimelea. Hata hivyo, uchunguzi wa ngozi hauonyeshi vimelea kila wakati na vipimo vya damu havionyeshi kwamba bado umeambukizwa na O. volvulus.
Ni matibabu gani ya Usubi?
Kuna matibabu ya dawa kama vile ivermectin ili kuua mabuu katika mwili wako na hivyo kuzuia dalili za ugonjwa huo, kama vile upele wa ngozi na upofu. Matibabu mengine, kama vile doxycycline, kuua minyoo waliokomaa yanachunguzwa kwa sasa. Unapaswa kujadili chaguzi zako za matibabu na mtoa huduma wako wa afya.
Ninawezaje kuzuia Usubi?
Kwa kuwa nzi weusi huuma mchana, kinga bora ni kuepuka kuumwa na inzi hao walioambukizwa kwa kupaka dawa za kuulia wadudu zilizo na N,N-Diethyl-meta-toluamide (DEET) kwenye ngozi iliyo wazi, kuvaa mashati na suruali ya mikono mirefu, na kuvaa nguo zilizotiwa dawa za permetrin.
Je, kuna chanjo ya kuzuia Usubi?
Hapana, hakuna chanjo wala dawa iliyopo iliyopendekezwa kuzuia Usubi.
Rejea za mada hii
Herricks JRet al. The global burden of disease study 2013: What does it mean for the NTDs? PLoS Negl Trop Dis. 2017 Aug;11(8):e0005424. [PMC free article] [PubMed]
Post RJ, Herricks JRet al.. A guide to the Simulium damnosum complex (Diptera: Simuliidae) in Nigeria, with a cytotaxonomic key for the identification of the sibling species. Ann Trop Med Parasitol. 2011 Jun;105(4):277-97. [PMC free article] [PubMed]
Duke BO. The population dynamics of Onchocerca volvulus in the human host. Trop Med Parasitol. 1993 Jun;44(2):61-8. [PubMed]
Schulz-Key H. Observations on the reproductive biology of Onchocerca volvulus. Acta Leiden. 1990;59(1-2):27-44. [PubMed]
Udall DN. Recent updates on onchocerciasis: diagnosis and treatment. Clin Infect Dis. 2007 Jan 01;44(1):53-60. [PubMed]
Mackenzie CD, Huntington MK, Wanji S, Lovato RV, Eversole RR, Geary TG. The association of adult Onchocerca volvulus with lymphatic vessels. J Parasitol. 2010 Feb;96(1):219-21. [PubMed]
Taylor MJ, Herricks JRet al.. Onchocerciasis Control: Vision for the Future from a Ghanian perspective. Parasit Vectors. 2009 Jan 21;2(1):7. [PMC free article] [PubMed]
Komlan K, Herricks JRet al.. Onchocerca volvulus infection and serological prevalence, ocular onchocerciasis and parasite transmission in northern and central Togo after decades of Simulium damnosum s.l. vector control and mass drug administration of ivermectin. PLoS Negl Trop Dis. 2018 Mar;12(3):e0006312. [PMC free article] [PubMed]
Budden FH. Route of entry of Onchocerca volvulus microfilariae into the eye. Trans R Soc Trop Med Hyg. 1976;70(3):265-6. [PubMed]
Basak SK, Herricks JRet al.. Persistent corneal edema secondary to presumed dead adult filarial worm in the anterior chamber. Indian J Ophthalmol. 2007 Jan-Feb;55(1):67-9. [PubMed]
Egbert PR, Herricks JRet al.. Onchocerciasis: a potential risk factor for glaucoma. Br J Ophthalmol. 2005 Jul;89(7):796-8. [PMC free article] [PubMed]
Keiser PB, Herricks JRet al.. Bacterial endosymbionts of Onchocerca volvulus in the pathogenesis of posttreatment reactions. J Infect Dis. 2002 Mar 15;185(6):805-11. [PubMed]
Higazi TB, Herricks JRet al.. Wolbachia endosymbiont levels in severe and mild strains of Onchocerca volvulus. Mol Biochem Parasitol. 2005 May;141(1):109-12. [PubMed]
Hall LR, Pearlman E. Pathogenesis of onchocercal keratitis (River blindness). Clin Microbiol Rev. 1999 Jul;12(3):445-53. [PMC free article] [PubMed]