
Ingawa matibabu kwa kutumia Misoprostol ni yenye ufanisi mkubwa, kuna uwezekano mdogo kwamba huenda mimba isitoke kabisa (takribani mwanamke 1 kati ya wanawake 100 anaweza kubaki mjamzito baada ya kutoa mimba kwa misoprostol.
Dalili zinazoashiria kwamba utoaji mimba haujafanikiwa kwa kutumia misoprostol
Haujatokwa na damu ndani ya masaa 24 baada ya kutumia Misoprostol.
Damu imetoka kwa muda wa chini ya siku 4 tu badala ya wiki moja au zaidi.
Bado unahisi dalili za ujauzito baada ya wiki moja ya kutumia dawa kama vile matiti kuuma, kichefuchefu, tumbo kuongezeka, n.k.
Baada ya wiki 2, unapofanya kipimo cha mkojo cha ujauzito , unapata majibu chanya(una mimba) au yasiyoeleweka.
Hedhi yako haijarudi ndani ya mwezi mmoja baada ya kutoa mimba.
Nini cha kufanya ikiwa una dalili hizi?
Ikiwa una moja ya dalili hizi, wasiliana mara moja na kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi. Unaweza kuhitaji dozi nyingine ya Misoprostol au njia nyingine za matibabu ili kuhakikisha ujauzito umetoka kabisa.
Namna ya kufahamu kama utoaji Mimba kwa misiprostol umefanikiwa
Utafahamu utoaji mimba kwa misoprostol kwamba umefannikiwa kwa:
Kupima ujauzito kwa kipimo cha mkojo wiki 2 baada ya matibabu. Kipimo hiki kitasoma kuwa hauna mimba. Ikiwa matokeo ni chanya au hayajaeleweka, tafuta msaada wa daktari haraka.
Fuata maagizo ya daktari ikiwa unahitaji matibabu ya ziada.
Rejea za mada hii
ULY CLINIC. Dalili za ujauzito. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ujauzito. Imechukuliwa 15.03.2025
ULY CLINIC. Misoprostol. https://www.ulyclinic.com/dawa/misoprostol-. Imechukuliwa 15.03.2025
Aid acess. Signs of incomplete abortion after misoprostol. https://aidaccess.org/en/page/461/how-do-you-know-if-you-have-an-incomplete-abortion. Imechukuliwa 15.03.2025