Je Kutokwa na ute wa njano baada ya kutoa mimba ni kawaida?
Je Mabadiliko gani hutokea kwenye ute baada ya kutoa mimba
Je ni lini ute utarejea kwenye rangi yake baada ya kutoa mimba?
Je niwe na hofu kama ute haujarejea kwenye rangi yake ya kawaida baada ya kutoa mimba?
Maswali hayo juu yamekuwa yakiulizwa sana na watumiaji wa tovuti ya ULY CLINIC. Makala hii imejikita kutoa majibu ya kitaalamu kuhusu ute baada ya kutoa mimba. Katika makala hii utapata majibu ya maswali yote hapo juu.
Hatua za mabadiliko ya ute baada ya kutoa mimba
Mara baada ya kutoa mimba, unaweza kutokwa damu mfululizo kwa muda wa hadi wiki moja ama kuwa na vipindi vya kuja na kuondoka vya kutokwa damu kwa muda wa wiki moja hadi 4.
Awali, kwa kuwa damu huwa ya kiasi hadi nyingi, ute unaotoka ukeni utakuwa na rangi nyekundu na wakati mwingine kuchanganyika na mabonge ya damu. Damu huweza kuongezeka kwenye ute endapo unafanya mazoezi na hupungua kwa kupumzika.
Baada ya wiki moja hadi 4 kupita, kiasi cha damu kwenye ute hupungua na hivyo mabadiliko katika ute hutokea. Ute huanza kuwa na vidoti vya damu, kuwa na rangi ya kahawia au rangi ya njano iliyokolea ambayo hupungua kwa siku zinavyoenda hadi kupata rangi yake ya kawaida.
Kwanini ute unakuwa wa njano baada ya kutoa mimba?
Ute unakuwa na rangi ya njano kutokana na kuchanganyika na damu kiasi.
Wakati gani uonane na daktari
Kutokwa na ute mwekundu ukeni uliochanganyika na mabonge makubwa mekundu au zambarau iliyokolea kwa zaidi ya siku 6 ni ishara ya kuhitaji uchunguzi wa haraka. Unapopata dalili kati ya hizi siku yoyote baada ya kutoa mimba fika hospitali haraka kwa uchunguzi na tiba.
Kizunguzungu
Kuzimia(kuzirai)
Degedege
Homa
Dalili hizi huweza maanisha umepoteza damu nyingi ama kupata maambukizi ukeni
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?
Soma zaidi kuhusu damu baada ya kutoa mimba kwa kubofya hapa
Unasauriwa pia kuwasiliana na daktari wako siku zote uonapo dalili yoyote ambayo huielewi kwa ushauri na tiba
Rejea za mada hii;
ULY CLINIC. Kutokwa Damu baada ya kutoa mimba. https://www.ulyclinic.com/foramu/majadiliano-na-wataalamu/kutokwa-damu-baada-ya-kutoa-mimba-kwa-dawa. Imechukuliwa 02.10.2024
UCSF. FAQ: Post-Abortion Care and Recovery. https://www.ucsfhealth.org/education/faq-post-abortion-care-and-recovery. Imechukuliwa 02.10.2024
Davis A, Westhoff C, De Nonno L. Bleeding patterns after early abortion with mifepristone and misoprostol or manual vacuum aspiration. J Am Med Womens Assoc (1972). 2000;55(3 Suppl):141-4. PMID: 10846324.
3. https://womenshealthclinic.org/what-we-do/abortion/after-an-abortion/. Imechukuliwa 25.01.2023
National Abortion Federation (2008) Early Medical Abortion; in Clinical Policy Guidelines Washington, DC; pp 7-11.
Breitbart V, Repass DC. The counseling component of medical abortion. J Am Med Womens Assoc
2000; 55(suppl 3):164-166.
Creinin MD. Randomized comparison of efficacy, acceptability and cost of medical versus surgical abortion. Contraception 2000; 62:117-24.
Henderson JT, Hwang AC, Harper CC et.al. (2005) Safety of mifepristone abortion in clinical use. Contraception 72:175-8.
Chen AY, Mottl-Santiago J, Vragovic O et.al. (2006) Bleeding after medication-induced termination of pregnancy with two dosing schedules of mifepristone and misoprostol. Contraception 73: 415-19.
Allen RH, Westhoff C, DeNonno L, Fielding SL, Schaff EA. Curettage after mifepristone-induced abortion: Frequency, timing, and indications. Obstet Gyncecol 2001;98:101-6.
Schaff EA, Fielding SL, Westhoff C, Ellertson C, Eisinger SH, Stadalius LS, Fuller L. Vaginal misoprostol administered 1, 2, or 3 days after mifepristone for early abortion. JAMA 2000;284:1948-1953.