Vidonge vya uzazi wa mpango huzuia mimba baada ya muda gani?
Dawa za uzazi wa mpango huzuia mimba baada ya kutumia kwa kuda gani au siku ngapi?
Ni lini dawa za mzazi wa mpango huanza kufanya kazi?
Siku ya ngapi baada ya kumeza dawa za uzazi wa mpango nitalindwa kupata ujauzito?
Kumeza dawa za uzazi wa mpango siku ya 1 ya kuona hedhi
Ukimeza kidonge mchanganyiko cha uzazi wa mpango siku ya 1 ya kipindi cha hedhi (siku ya 1 ya mzunguko wako wa hedhi) itazuia kupata mimba mara moja. Hutahitaji kutumia njia ya ziada ya uzazi wa mpango.
Kumeza dawa za uzazi wa mpango siku ya 5 ya mzunguko wako au kabla
Ukianza kutumia kidonge siku ya 5 ya kuona damu ya hedhi au kabla, dawa itazuia kupata ujauzito mara moja.
Kumeza dawa za uzazi wa mpango baada ya siku ya 5 ya mzunguko wako
Hutalindwa kutokana na mimba mara moja na utahitaji uzazi wa mpango wa ziada hadi utakapokuwa umemeza kidonge kwa siku 7.
Ikiwa utaanza kidonge baada ya siku ya 5 ya mzunguko wako, hakikisha kuwa hujashiriki ngono tangu hedhi ya mwisho. Ikiwa una wasiwasi kuwa una mjamzito unapoanza kutumia kidonge, fanya kipimo cha ujauzito wiki 3 baada ya mara ya mwisho kufanya ngono bila kinga.
Rejea za mada hii
Oral contraceprives. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430882/. Imechukuliwa 17.04.2023
Hall KS, Trussell J, Schwarz EB. Progestin-only contraceptive pill use among women in the United States. Contraception. 2012 Dec;86(6):653-8. doi: 10.1016/j.contraception.2012.05.003. Epub 2012 Jun 6. PMID: 22682722; PMCID: PMC3440515.
Grimes DA, et al O'Brien PA, Raymond EG. Progestin-only pills for contraception. Cochrane Database Syst Rev. 2010:CD007541. [PubMed].
Sheth A, et al. A randomized, double-blind study of two combined and two progestogen-only oral contraceptives. Contraception. 1982;25:243–52. [PubMed]