Swali
Je vifaa vya kujifungulia ni vipi?
Je, natakiwa kuandaa vifaa gani kabla ya kwenda kujifungua?
Majibu
Vifaa vya kujifungulia ni nyenzo muhimu zinazokuwezesha kujifungua salama na kupatamatunzo muhimu kwako na mtoto. Kwenye baadhi ya hosptiali, itakupasa kuwa na vifaa vyako vya kujifungulia kutokana na uhaba wa vifaa hivyo, haswa kwenye hospitali ambapo wamama wengi hujifungua.
Orodha ya vifaa vya kujifungulia
Baadhi ya vifaa vya kujifungulia huwa pamoja na;
Mipira ya kuvaa mikononi ( Glavu za upasuaji)
Mpira wakutandika (Makintoshi)
Kibana kitovu cha kichanga
Kisu cha upasuaji
Bando la pamba
Pedi za mzazi
Mabomba ya sindano yenye ujazo wa 2cc na 5cc
Dawa ya kuchoma aina ya tranexamic
Nguo za kufunika mtoto
Wapi utapata vifaa hivi vya kujifungulia?
Vifaa hivi vya kujifungulia unaweza vipata katika maduka ya dawa na vifaa tiba. Kumbuka wakati wa kununua ni vema ukamwambiua muuzaji akupe seti nzima ya vifaa vya kujifungulia kama itakuwepo ili kuepuka ununuzi wa kifaa kimoja moja.
Wapi utapata maelezo zaidi kuhusu vifaa vya kujifungulia?
Pata maelezo zaidi kutoka kwa daktari wako au mtoa huduma yeyote wa afya ambaye atakuhudumia wakati wa kujifungua ili ufahamu ni vifaa vipi muhimu utapaswa kuwa navyo.