Matumizi ya energy drink
Madhara ya kutumia energy drink
Kisa cha mtu aliyekufa kutokana na enegry drinki
Madhara ya kutumia kwa wingi vinywaji vya kutia nguvu
Madhara ya kutumia vinywaji vya kuongeza nguvu
Energy drinki kwenye afya
Mwanaume wa miaka 28 mwenye asili ya kiafrika alipelekwa hospitali ya Jakaya Kikwete akiwa na tatizo la maumivu ya kifua lililoanza masaa 8 kabla ya kuwasili hospitali. Dalili alizokuwa nazo ni maumivu nyuma ya kifua yaliyoambatana na kuishiwa pumzi na kutokwa jasho jingi yaliyoanza masaa 4 baada ya kunywa enegry drinki 5 ambayo ina viungo vya kafeini, taurine, glukosi, glucuronolactone.
Uchunguzi wa historia
Kijana huyu hakuwa na historia iliyopita ya ugonjwa au tatizo la moyo wala kuwa na kihatarishi cha ugonjwa wa moyo.
Uchunguzi wa awali wa mwili
Uchunguzi wa awali wa mwili haukuonyesha kiashiria cha tatizo lolote mwilini.
Uchunguzi wa vipimo
Vipimo vya picha na umeme wa moyo vilionyesha ishara ya kuziba kwa mishipa midogo inayolisha kuta za moyo na hivyo kuonyesha kuwa shida iliyokuwa inamsumbua ni ugonjwa mkali wa koronari ambao kwa hapa unajulikana kama mayokadia infaksheni.
Magonjwa yanayotokana na matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu
Magonjwa yanayohusianishwa na utumiaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu vikifahamika pia kama energy drink mara nyingi ni magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, magonjwa ya mfumo wa homoni za endokrini, mfumo wa fahamu, chakula na figo. Baadhi ya magonjwa ya moyo ni:
Mayokadia infaksheni.
Kupasuka kwa mshipa wa aota.
Kuziba kwa mishipa ya koronari.
Takotsubo kadiomayopathi.
Kifo cha ghafla cha mayokadia.
Kwanini kujali kuhusu kudhibiti matumizi ya vinjwaji vya kuongeza nguvu?
Magonjwa ya moyo kama aliopata kijana huyu ambayo awali yalikuwa yanatokea kwa wazee kwa sababu ya mabadikiko katika mishipa ya damu na ufanyajikazi wa mfumo huo damu na moyo, kwa sasa yanaongezeka kwa kasi kwa vijana wadogo na matibabu yake ni magumu. Magonjwa haya yanayoua na kupoteza nguvu kazi ya taifa huzuilika kwa kuacha au kupunguza utumiaji wa vyakula au vinywaji vya jamii hiyo ambavyo bila wao kufahamu wanadhani kuwa ni bora kwa starehe.
Matokeo ya vinywaji vya kutia nguvu mwilini.
Vinywaji vya kutia nguvu kwa kuwa huwa na sukari ya carbohydrate kwa wingi, vinapoingia kwenye damu, mwili huitikia kwa kuchochea tezi kongosho kuzalisha kichocheo insulin kwa wingi. Kichocheo hiki hufanya kazi kubwa ya kuchochea chembe hai kutumia sukari ya glukosi ili kuzalisha nishati kukidhi mahitaji ya mwili yaliyopo mfano nguvu ya misuli kufanya kazi ili ulime au nguvu ya ubongo kufikiria unaposoma n.k. Endapo kiwango cha sukari kilichoingia ni kingi kuliko mahitaji, homoni hii hubadilisha glukosi kuwa glaikojeni na kuihifadhi kwenye ini ama kuwa mafuta kisha kuhifadhiwa kwenye tishu zinazohifadhi mafuta zinazopatikana kwenye tumbo, makalio, mapaja, shingo ,mabega n.k. Baadhi ya mafuta hutuwama katika mishipa ya damu hivyo kupunguza kipenyo chake ama kuziba kabisa. Mafuta haya hufanya mishipa hiyo kuwa dhaifu na kushindwa kufanya kazi yake kiasi cha kuketa magonjwa mbakimbali ya moyo na mishipa ya damu. Ufanyaji kazi wa kupitiliza wa kongosho hupelekea lishindwe kuzalisha insulin na hivyo kusababisha ugonjwa wa kisukari cha watu wazima.
Ushauri
Vijana wanapaswa kula mlo kamili na vinywaji asili kutoka kwenye vyakula asili kulingana na mahitaji ya mwili. Endapo kuna uhitaji wa haraka kuongeza nguvu mwilini, vinywaji jamii hii vinaweza kuwa msaada kwa wakati huo tu na si kutumika kama kiburudisho.
Rejea za mada hii:
Grasser EK, et al. Energy drinks and their impact on the cardiovascular system: potential mechanisms. Adv Nutr. 2016;7(5):950-960.
Alsunni AA. Energy drink consumption: beneficial and adverse health effects. Int J Health Sci. 2015;9(4):468-474.
Energy drinks market size, share & trends analysis report by product (drinks, shots, mixers), by type (conventional, organic), by packaging (cans, bottles), by Distribution Channel, by Region, and Segment Forecasts, 2022-2030. https://www. researchandmarkets.com/reports/4375425/energy-drinks-market-size-share-and-trends
Higgins JP, et al. Acute coronary syndromes in Sub-Saharan Africa: a 10-year systematic review. J Am Heart Assoc. 2022;11(1):e021107.
Garoufalis S, et al. Comparison of angiographic findings, risk factors, and long term follow-up between young and old patients with a history of myocardial infarction. Int J Cardiol. 1998;6(1):75-80.
Fournier JA, et al. Myocardial infarction in men aged 40 years or less: a prospective clinical-angiographic study. Clin Cardiol. 1996;19(8):631-636.
Doughty M, et al. Acute myocardial infarction in the young–The University of Michigan experience. Am Heart J. 2002;143(1):56-62.
Greenland P, et al. In-hospital and 1-year mortality in 1,524 women after myocardial infarction. Circulation. 1991;83(2):484-491.
Gulati R, et al. Acute myocardial infarction in young individuals. Mayo Clin Proc. 2020;95(1):136-156.
Shah N, et al. Myocardial infarction in young versus older adults: an analysis of differences in proportion, risk factors, clinical demographics, angiographic findings and in-hospital outcomes. Int J Clin Cardiol. 2016;3:079.
Shah SS, Noor L, Shah SH, Din SU, Awan ZA, Hafizullaht M. Myocardial infarction in young versus older adults: clinical characteristics and angiographic features. J Ayub Med Coll Abbottabad. 2010;22(2):187-190.
Anh DT, et al. Age related differences in acute coronary syndrome: an observation at a central hospital in Vietnam. J Transl Int Med. 2021;9(1):32-37.
Al-Shahrani MS, et al. Differences in clinical nature and outcome among young patients suffering from an acute coronary syndrome. J Blood Med. 2021;12:10111017.
Bush N, et al. Comparison of demographic profile, risk factors, and in-hospital outcome in young and old patients with acute coronary syndrome: a single-center experience. J Family Med Prim Care. 2021;10(2):871-876.
Hertz JT, et al. Acute myocardial infarction in Sub-Saharan Africa: the need for data. PLoS ONE. 2014;9(5):e96688.