Virusi vya UKIMWI vinaweza kuishi muda wa saa 1 hadi siku 42 ikitegemea mambo yafuatayo
Idadi ya virusi
Wingi wa damu au kiwango cha damu na majimaji yenye virusi
Joto la mazingira
Unyevu kwenye hewa
Mwanga wa jua
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi kwenye sindano ya tundu
Virusi vinaweza kuishi muda mrefu zaidi kwenye sindano ya kuchomea dawa endapo joto na hali ya hewa havibadiliki badiliki. Mfano endapo sindano imewekwa kwenye jokofu, virusi vilivyo kwenye sindano vinaweza kuishi hadi siku 42.
Endapo sindano hii ipo kwenye joto la mazingira, virusi vya UKIMWI vinaweza kuishi muda wa siku 7.
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye manii/shahawa
Mara baada ya mbegu za kiume kutoka nje ya mwili, huanza kufa mara moja kutokana na kupigwa na hewa pamoja na joto la mazingira. Hivyo inachukua saa1 hadi 2 kuwa havina uwezo wa kuambukiza endapo mbegu hizo zimekauka kabisa.
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi kwenye damu iliyo kwenye mazingira
Asilimia 90 hadi 99 ya virusi hufa ndani ya masaa kadhaa baada ya damu au majimaji kupigwa na hewa, mwanga wa jua au kukauka katika joto la mazingira.
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye maji
Virusi vya UKIMWI endapo vitawekwa kwenye maji huchukua muda wa masaa nane (8) kupoteza uwezo wake wa kuambukiza (hufa). Hata hivyo ndani ya masaa mawili (2) kwenye maji, ni asilimia 10 tu ya virusi vinaweza kuishi, muda unavyoongezeka idadi a virusi huwa 0 baada ya masaa 8.

Rejea za mada hii
Recommendations for Prevention of HIV Transmission in Health-Care Settings.https://www.cdc.gov/MMWR/preview/MMWRhtml/00023587.htm. Imechukuliwa 14.06.2021
CDC. HIV transmission. https://www.cdc.gov/hiv/basics/transmission.html. Imechukuliwa 14.06.2021
N Abdala, et al. Survival of HIV-1 in syringes: effects of temperature during storage. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10921429/. Imechukuliwa 14.06.2021
Blood-borne viruses and their survival in theenvironment: is public concern about communityneedlestick exposures justified?. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/epdf/10.1111/j.1467-842X.2003.tb00606.x. Imechukuliwa 14.06.2021