
Wiki za kujifungua katika makala hii imemaanisha wiki ambapo endapo utajifungua mtoto atakuwa na afya njema na kuishi bila kuhitaji usahidizi au uangalizi mkubwa. Kwa kawaida wastani wa umri wa ujauzito ni wiki 40, hata hivyo mwili wa mwanamke na mji wake wa mimba huweza kuamua ujauzito uishie muda gani. Kwa wanawake wengi, wastani wa muda wa kujifungua ni kati ya wiki ya 37 hadi 42. Kujifungua katika kipindi hiki ni salama.
Maelezo ziaida ya wiki za kujifungua ni ngapi?
Yafuatayo ni maelezo ya ziada kuhusu wiki salama ya kujifungua
Muda kamili wa ujauzito: Wiki 39 hadi 40 na siku 6
Huu ndio muda mzuri zaidi kwa ukuaji wa ubongo, mapafu, na ini unakuwa umekamilika na hivyo hatari ya matatizo ya kujifungua kwa mama na mtoto huwa ndogo sana.
Muda kamili wa awali: Wiki 37 hadi 38 na siku 6
Baadhi ya watoto wanaweza kuwa na changamoto ndogo za kupumua au kunyonya wakizaliwa katika wiki hizi, inapendekezwa na madaktari wengi kusubiri hadi angalau wiki 39 isipokuwa kama kuna sababu ya kitabibu.
Muda kamili wa kuchelewa: Wiki 41 hadi 41 na siku 6
Katika muda huu, bado ni salama kujifungua mtoto lakini huhitaji uangalizi zaidi kutokana na hatari kama kupungua kwa maji katika chupa ya uzazi. Jinsi mtoto anavyochelewa kutoka kiasi cha maji hupungua kutokana na kunywa maji hayo na kupungua kwa uzalishaji wake.
Muda kamili wa kuchelewa kupita kiasi (Hatari zaidi): Wiki 42 na zaidi
Kuna hatari kubwa ya matatizo kama kushindwa kufanya kazi vizuri kwa kondo la nyuma au mtoto kujisaidia tumboni na kupelekea kuvuka kinyesi hicho katika mfumo wa hewa. Hali hii ni hatari kwa afya ya mtoto kiasi vha kumpelekea kupoteza maisha kama hatua za haraka zisipochukuliwa.
Hitimisho
Kwa matokeo bora kiafya, kujifungua kunatakiwa kutokea katika wiki ya 39-40, katika kipindi hiki ni salama zaidi kujifungua kama uchungu umeanza wenyewe isipokuwa kama kuna sababu ya kitabibu ya kujifungua mapema.
Rejea za mada hii
ACOG. Definition of term birth. https://www.acog.org/clinical/clinical-guidance/committee-opinion/articles/2013/11/definition-of-term-pregnancy Imechukuliwa 15.03.2025
Fleischman AR, et al. Rethinking the definition of "term pregnancy". Obstet Gynecol. 2010 Jul;116(1):136-139. doi: 10.1097/AOG.0b013e3181e24f28. PMID: 20567179.
Galal M,et al. Postterm pregnancy. Facts Views Vis Obgyn. 2012;4(3):175-87. PMID: 24753906; PMCID: PMC3991404.
Iams JD. Prediction and early detection of preterm labor. Obstet Gynecol. 2003 Feb;101(2):402-12.
ACOG Practice Bulletin No. 107: Induction of labor. Obstet Gynecol. 2009 Aug;114(2 Pt 1):386-397.
Martin JA, et al: Final Data for 2017. Natl Vital Stat Rep. 2018 Nov;67(8):1-50.
Gregory KD,et al. Cesarean versus vaginal delivery: whose risks? Whose benefits? Am J Perinatol. 2012 Jan;29(1):7-18.
Zhang J, et al. The natural history of the normal first stage of labor. Obstet Gynecol. 2010 Apr;115(4):705-710.
Le Ray C, et al. PREMODA Study Group. Duration of passive and active phases of the second stage of labour and risk of severe postpartum haemorrhage in low-risk nulliparous women. Eur J Obstet Gynecol Reprod Biol. 2011 Oct;158(2):167-72.