top of page

Gesi kujaa tumboni

 

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

Dalili hii ya hisia ya tumbo kujaa gesi mara nyingi husababishwa na ulaji wa vyakula aina fulani, hata hivyo kunabaadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha tatizo hili. Ingawa watu wengi hufahamu kwamba kujaa kwa tumbo  kunaweza kusababishwa na kula maharage, ama vitunguu ila ni muhimu kutambua kwamba vyakula kama maziwa, matunda aina kadhaa, soda viazi vitamu na viazi mviringo vya kuchemsha mahindi ya kuchemsha na kuchoma na pilau huweza kusababisha tatizo la tumbo kujaa gesi.

Sukari aina ya fructose inayopatikana kwenye matunda na soda pamoja na lactose inayopatikana katika maziwa na vyakula vya kusindikwa huwa visababishi vikuu vingine vya tumbo kujaa gesi, maumivu ya tumbo na kuhara.

Tatizo la kujaa kwa tumbo linaweza kusababishwa na magonjwa mengine kama yafuatayo;

 

  • Irritable bowel syndrome

 

Ugonjwa huu hutokea kutokana na mvurugiko wa mfumo wa tumbo,huwa ni vigumu sana kugunduliwa na madakitari kwa sababu dalili zake hufanana na magonjwa mengine

 

  • Magonjwa wa inflamatori baweli

  • Madhaifu ya tumbo, kama kuziba kwa tumbo, na kukosekana kwa mijongeo ya misuli ya tumbo

  • Konstipesheni

  • Kiungulia

  • Kutohimili vyakula vyenye sukari ya fructose

  • Kuongezeka uzito

  • Mabadiliko ya homoni kwa wanawake

  • Maambukizi ya giardia

  • Madhaifu ya kula chakula kama bulimia na anoreksia nevosa

  • Magonjwa ya akili kama msongo wa mawzo, hofu na huzuniko kuu

  • Baadhi ya dawa​ kama ibuprofen, naproxen, matumizi ya antibayotiki, hydrocodone, dawa za kushusha kiwango cha kolestro kwenye damu kama simvastatin na atovastatin, madini chuma na dawa za kutibu saratani

Dalili zifuatzo huweza kuambatana na ugonjwa huu

  • Tumbo kujaa gesi

  • Kujaa kwa tumbo

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuhisi mvurugiko katika tumbo

  • Kukosa choo kwa muda wa wiki moja na kufuatiwa na kuhara wiki inyofuata

Hakuna kisababishi halisi kinachosababisha ugonjwa huu ila kuna vihatarishi vinavyofahamika vinachangia kuamsha tatizo hili kama vile

  • Msongo wa mawazo

  • Kuharibika kwa mfumo wa vichochezi mwili

  • Kuharibika kwa mfumo wa fahamu wa ubongo

  • Kutafuna bablishi/bigijii, hii husababisha kuingia kwa gesi kwenye tumbo

  • Kunywa au Kutafuna chakula haraka haraka

Matumbo ya mtu huwa hayana tatizo lolote na  mwathilika huwa mzima katika mfumo wa chakula, dalili za ugonjwa huu maranyingi huwa mbaya wakati wa jioni. Cha kusikitisha ni kwamba hakuna tiba kwa ajili ya kuondoa kabisa tatizo hili, kinachofanyika ni kupunguza dalili na kubadili mfumo wa maisha tu

  • Kupunguza ulaji wa vyakula vya nyuzinyuzi zinazotokana na vyakula vya mbegu huweza kusaidia kupunguza dalili za tatizo hili kwa asilimia 20 hadi 30

  • Zuia kula mikate, ngano, biskuti , vitumbua, maandazi

  • Usitafune bablishi

  • Zuia kula vyakula vya kusindikwa vilivyotiwa kaboni kama vile soda na juisi za kusindikwa.

  • Kula chakula taratibu na usinywe maji katikati ya mlo wa chakula

  • Acha kutumia vyakula vyenye lactose kama maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa

  • Kufanya masaji ya tumbo

ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ili dhidi ya afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa elimu na ushauri kupitia namba za simu au kubonyeza Pata Tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa mara ya mwisho 7/05/2020

Rejea za mada hii

bottom of page