top of page

Magonjwa

Public·783 members

Sumu ya kunywa maji mengi kupita kiasi

Kunywa maji mengi kupitiliza

Haishauriwi kiafya kunywa maji mengi zaidi ya mahitaji ya mwili wako kwa kuwa kiwango kinachozidi huweza geuka kuwa sumu. Kwa bahati mbaya dalili za sumu ya maji kutokana na kunywa maji mengi huwa ngumu kutambuliwa kirahisi na wataalamu wa afya kwa kuwa dalili zake hufanana na magonjwa ya akili, endapo tatizo lisipofahamika mapema na kupata tiba huleta madhara makubwa pamoja na kifo.

 

Tatizo la sumu ya maji linalotokea kutokana kuwa na maji mengi mwilini kuliko kiwango cha chumvi hutokea kwa nadra na huweza pelekea kifo.

 

Dalili za mtu aliyekunywa maji mengi kupitiliza

Utambuzi wa mtu aliyeathirika na maji huwa si rahisi kutokana na dalili zake kuhusiana na matatizo mengine yanayoweza kufikiriwa kuwa ugonjwa wa akili.

  • Kama mtu akinywa maji mengi kupitiliza kwa haraka anaweza kupata dalili za awali zifuatazo;

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuchanganyikiwa au kuchanganya mambo

  • Maumivu ya kubana kwa misuli

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Kuvimba mwili, miguu mikono na tumbo


Dalili za baadae za kunywa maji mengi kupita kiasi

Dalili za baadae zinazoashiria tatizo kuwa kubwa zaidi huwa pamoja na:

  • Kupata hisia ya kutopendwe au kukubalika

  • Kupata hisia zisizo halisi na imani potofu

  • Kuona vitu visivyoonekana na watu wengine

  • Kusikia sauti zisizosikiwa na watu wengine

  • Kuchanganyikiwa( Kukanganya mambo)

  • Kupoteza fahamu

  • Kutambulika huwa muhimu ili kuzuia dalili zingine za degedege na kuzimia. Tatizo lisipogundulika linaweza kupelekea kifo.

 

Visababishi vya kunywa maji mengi kupita kiasi

Licha ya tatizo kutokea kwa nadra sana, sumu ya maji inaweza kusababishwa na sababu mbalimbali ambazo ni;

  • Mazoezi: kunywa maji mengi baada ya mazoezi ya muda mrefu pasipo kurejesha madini yaliyopotea kwenye jasho

  • Kunywa maji mengi kutokana na matatizo ya kisaikolojia ya kupata kiu kupitiliza

  • Kunywa maji ya kutosha kama adhabu au kwenye mashindano

  • Kuishiwa maji kwenye hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha homoni (ADH)

  • Kufanya kazi kwenye hali ya hewa ya joto

  • Matumizi ya dawa kama dawa zinazoongeza kiu kama vile dawa za magonjwa ya akili au usumu wa dawa jamii ya NSAIDS na dawa za kupunguza maji mwilini

  • Magonjwa ya figo yanayopelekea kutochunjwa vema kwa maji

  • Ugonjwa wa ini na Schizophrenia

  • Kuferi kwa moyo


Mambo ya kufanya ili usizidishe kiwango cha maji

  • Kunywa maji kulingana na kiu unayopata na hali yako ya kiafya, usinywe zaidi ya lita moja kwa saa au kujilazimisha

  • Chunguza rangi ya mkojo unayopata wakati wa kukojoa, mkojo unapaswa kuwa wa njano mpauko. Kama una rangi ya maji inaweza kuonyesha umekunywa maji mengi hivyo usiendelee mpaka utakapopata kiu.

  • Acha kunywa maji kama unajisikia kichefucehfu na kutapika au maumivu ya kichwa- dalili hizi ni dalili za awali za kuwa na maji mengi mwilini.

  • Acha kunywa maji endapo kiu imekata

  • Jifunze kuusikiliza mwili wako unataka maji au la.

 

Madhara ya kunywa maji mengi kupita kiasi

  • Degedege

  • Kupoteza fahamu

  • Kifo


Rejea za mada hii:

  1. Lee LC, Noet al. When Plenty Is Too Much: Water Intoxication in a Patient with a Simple Urinary TractI nfection (https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5129180/)BMJ Case Rep. 2016 Nov 1;2016:bcr2016216882. Imechukuliwa 29.10.2024

  2. Merck Manual Consumer Version. Overhydration (https://www.merckmanuals.com/home/hormonal-and-metabolic-disorders/water-balance/overhydration). Last reviewed 5/2024. Imechukuliwa 29.10.2024

  3. Peechakara BV, e tal.  Water Toxicity (https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537231/). 2023 Jun 26. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island, FL: StatPearls Publishing; 2024 Jan. Imechukuliwa 29.10.2024

  4. Renal Function & Micturition. In: Barrett KE, et al, eds. Ganong’s Review of Medical Physiology. 26th ed. McGraw-Hill Education; 2019.

  5. Siegel AJ. Fatal water intoxication and cardiac arrest in runners during marathons: prevention and treatment based on validated clinical paradigms. Am J Med. 2015 Oct;128(10):1070-5.

  6. Umansky L, Sella A. [Psychogenic polydipsia leading to water intoxication]. Harefuah. 2000 Jan 02;138(1):9-12, 87. 

  7. Water intoxication. https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/water-intoxication. Imechukuliwa 29.10.2024

9 Views

About

Sehemu ambayo imeandikwa magonjwa mbalimbali yanayowapata bi...

bottom of page