Njia bora za kuthibitisha kama mimba imetoka
Swali la msingi
Habari daktari. Ukishatoa mimba kwa dawa unawezaa kupima tena kwa kutumia kipimo Cha mkojoo ilikujua kamaa imetoka?
Majibu
Habari! Asante kwa swali zuri.

Baada ya kutoa mimba kwa kutumia dawa (medical abortion), kutumia kipimo cha mimba cha mkojo si njia sahihi kabisa ya kuthibitisha kama mimba imetoka yote. Hii ni kwa sababu: Homoni ya ujauzito-HCG (inayopimwa kwenye mkojo) inaweza kubaki mwilini kwa wiki kadhaa baada ya kutoa mimba, hata kama mimba imetoka yote. Hivyo kipimo cha mkojo kinaweza kuendelea kuonyesha matokeo chanya (mimba ipo) hata baada ya wiki 3–4 baada ya kutoa mimba, ingawa mimba haipo tena.
Njia bora za kuthibitisha kama mimba imetoka yote
Zifuatazo ni njia bora za kutambua kama mimba imetoka yote;
Uchunguzi wa daktari – Kupitia dalili na vipimo, kama uchungu wa tumbo, damu inayoendelea kutoka, au dalili nyingine.
Kipimo cha picha ya tumbo – Hii ndiyo njia sahihi zaidi ya kuthibitisha kama mfuko wa uzazi hauna mabaki ya mimba.
Kupungua kwa dalili za ujauzito – Kama kichefuchefu, uchovu, na matiti kujaa huanza kupungua au kuisha.
Ushauri
Mara baada ya kutumia dawa ya kutoa mimba, ni vyema kurudi kituo cha afya baada ya siku 7–14 kwa uchunguzi wa kuthibitisha kama mimba imetoka yote na hakuna mabaki ambayo yanaweza kusababisha maambukizi au matatizo mengine.
Wakati gani wa kuonana na daktari?
Onana na daktari haraka ikiwa una dalili zifuatazo;
Maumivu makali ya tumbo
Damu nyingi isiyoisha
Homa au harufu mbaya kutoka ukeni
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Medical management of abortion. Geneva: WHO; 2018.
Raymond EG, Harrison MS, Weaver MA. Efficacy of misoprostol alone for first-trimester medical abortion: a systematic review. Obstet Gynecol. 2019;133(1):137–47.
Upadhyay UD, Desai S, Zlidar V, Weitz TA, Grossman D, Anderson P, Taylor D. Incidence of emergency department visits and complications after abortion. Obstet Gynecol. 2015;125(1):175–83.
Goyal V. Medical abortion in primary care. J Fam Pract. 2021;70(4):185–92.
American College of Obstetricians and Gynecologists. Clinical guidelines: Medication abortion up to 70 days of gestation. ACOG; 2020.
Grossman D, Grindlay K. Alternatives to ultrasound for follow-up after medication abortion: a systematic review. Contraception. 2011;83(6):504–10.
Ngo TD, Park MH, Shakur H, Free C. Comparative effectiveness, safety and acceptability of medical abortion at home and in a clinic: a systematic review. Bull World Health Organ. 2011;89(5):360–70.