Mwandishi: ULY CLINIC
Mhariri: Benjamin L, MD
Imeandikwa 3.03.2017
Harufu mbaya sehemu ukeni
Harufu kwenye uke ni harufu yoyote ile inayotokea kwenye uke. Ni kitu cha kawaida kwa uke wako kuwa na harufu kidogo ya kawaida lakini harufu kali/mbaya inayotokea kwenye uke na haswa kama vile harufu ya samaki huweza kuashiria kunatatizo kwenye uke.
Dalili zinazoweza kuamabtana na harufu mbaya ukeni
Harufu mbaya huweza kuambatana na dalili nyingine kama vile:
-
Hisia za kuungua sehemu za siri
-
Uvimbe wa michomo kinga
-
Kutokwa uchafu sehemu ukeni
Visababisi vya harufu mbaya ukeni
Vifuatavyo ni baadhi ya visababishi vya harufu mbaya ukeni
Kuingia hedhi Hedhi
Harufu kwenye uke hutofautiana wakati unapokuwa kwenye siku za hedhi na unapokuwa haupo kwenye siku zako.
Tendo la ndoa
Mwanamke anaweza kuhisi harufu isiyo ya kawida baada ya tendo la ndoa.
Jasho maeoeo ya ukeni
Jasho la kawaida pia linaweza kusababisha harufu kwenye uke.
Kujisafisha sana na kupaka kemikali kali ukeni
Wakati mwingine unaweza kujaribu kujisafisha sana ndani ya uke na kupaka manukato yanayozuia harufu, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa sababu manukato haya huongeza michomo na kusababisha kuonekana kwa dalili zingine ukeni.
Ongezeko la bakteria rafiki ukeni
Kuzidi kwa bakteri rafiki ukeni (wanaofahamika kama Gardnerella vaginalis) kutokana na kupungua kwa bakteria walinzi ukeni (Lactobacillus) hupelekea pia harufu mbaya ukeni.
Maambukizi ya trichomoniasis
Maambukizi ya Trichomoniasis- moja ya ugonjwa wa zinaa husababisha pia harufu ukeni mithiri ya samaki aliyeoza.
Usafi duni ukeni
Uke usiposafishwa vema, mkusanyiko wa majimaji na jasho hutengeneza harufu mbaya ukeni. Inahsauriwa kujisafisha kwa maji safi tu bila kutumia sabuni kali.
Kuvaa taulo ya kike(pedi) kwa mda mrefu
Pedi inapopata damu au jasho, bakteria hupenda hali hiyo na hivyo kujizalia kwao katika damu na jasho huweza tengeneza harufu mbaya ukeni.
Kumbuka
-
Kwa ujumla kama unaharufu ukeni na haiambatani na dalili zingine tajwa hapo juu basi, harufu hiyo si kitu kisicho cha kawaida.
-
Maambukizi ya kaswende, kisonono na fangasi ukeni huwa hayasababishi harufu mbaya ukeni.
Visababishi vingine
Kwa nadwa sana harufu ukeni inaweza kusababishwa na sababu zifuatazo(bofya makala husika kusoma zaidi);
Rejea za mada hii
-
NCBI. Bacterial Vaginosis. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK459216/#. Imechukuliwa 10.03.2025
-
Mayo Clinic. Vaginal fistula. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/vaginal-fistulas/symptoms-causes/syc-20355762. Imechukuliwa 10032025
-
Greenbaum S, Greenbaum G, Moran-Gilad J, Weintraub AY. Ecological dynamics of the vaginal microbiome in relation to health and disease. Am J Obstet Gynecol. 2019 Apr;220(4):324-335.
-
Russo R, Karadja E, De Seta F. Evidence-based mixture containing Lactobacillus strains and lactoferrin to prevent recurrent bacterial vaginosis: a double blind, placebo controlled, randomised clinical trial. Benef Microbes. 2019 Feb 08;10(1):19-26.
-
Deese J, Pradhan S, Goetz H, Morrison C. Contraceptive use and the risk of sexually transmitted infection: systematic review and current perspectives. Open Access J Contracept. 2018;9:91-112.
-
Javed A, Parvaiz F, Manzoor S. Bacterial vaginosis: An insight into the prevalence, alternative treatments regimen and it's associated resistance patterns. Microb Pathog. 2019 Feb;127:21-30.
-
Hartmann AA. [Gardnerella vaginalis infection. Clinical aspects, diagnosis and therapy]. Urologe A. 1987 Sep;26(5):252-5.
-
NBCI. VAGINAL DISCHARGE SYNDROME. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK572663/. Imechukuliwa 10032025
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri na tiba kutoka kwa daktari kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu chini ya tovuti hii au kwa kubonyeza Pata tiba
Imeboreshwa 10/03/2025