Harufu mbaya kinywani/mdomoni-tatizo la mdomo kunuka
Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Harufu mbaya ya kinywa kwa lugha nyingine huitwa halitosis huweza kusababishwa na;
-
Chakukula aina Fulani,
-
Magonjwa ya kinywa na
-
Tabia ya mtu
Kwa watu wengi harufu ya kinywa/mdomo huweza kuisha endapo mtu anazingatia usafi wa kinywa chake. Endapo matunzo yasiyo na gharama ya kinywa yamekushinda basi unaweza kumtafuta daktari wa meno ama daktari wa magonjnwa ya kawaida kwa matibabu zaidi na uchunguzi, na kufahamu kama kuna tatizo linalosababisha kupata harufu kinywani.
Ni vigumu kujijua kama unatoa harufuu mbaya mdomoni kwa sababu unakuwa ushazoea harufu hiyo, waulize wenzako kuhusu harufu ya kinywa chako na watakujibu vema kuliko kujihisi mwenyewe kwa sababu wakati mwingine unaweza usiwe na harufu mdomoni lakini ukawa unahisi kuwa unato harufu mdomoni.
​
Nini husababisha harufu mbaya kinywani/mdomoni?
Harufu mbaya kinywani mara nyingi huanzia kwenye mdomo, kuna sababu nyingi sana zinazosababisha kutoa harufu kinywani kama vile;
Chakula: bakteria wanapenda majimaji na mabaki ya chakula yanayoachwa baada ya kula chakula, bacteria hao husababisha harufu kinywani. Chakula kama vitunguu maji, pilipili na vitunguu swaumu pia huleta harufu mbaya kinywani.baada ya mmengenyo wa chakula hiko kufanyika katika kinywa na kuingia katika mfumo wa damu husafili na kufika katika mapafu pia na kutolewa kwa njia ya hewa na hivo kuchangia kuleta harufu mbaya ya kinywani.
Tumbaku na mazao ya tumbaku: tumbaku pekee huleta harufu ya pekee kinywani na huchangia kwenye uharibifu wa meno na fizi, magonjwa ya fizi na meno huchangia kutoa harufu mbaya kinywani.
Uchafu katika kinywa: kama usipopiga mswaki kinywa chako na kusukuta kwa maji, mabaki ya chakula hubaki kwa kwenye uwazi wa meno na fizi na huchangia kuleta harufu kwa sababu bakteria hukua kwenye mabaki hayo. Pili bakteria wanapokuwa husababisha kutengeneza ute unaofunika fizi na meno na kisha husababisha maambukizi kwenye meno na fizi ambapo madhara yake ni kuleta harufu mbaya kinywani.
​
Kinywa kikavu: mate husaidia kuosha uchafu unaosababisha harufu mbaya, hali kama ya ugonjwa inayosababisha kinywa kuwa kikavu/ mdomo kuwa mkavu kwa lugha nyingine xerostomia huchangia katika kusababisha harufu mbaya kinywani. Kinywa kuwa kikavu kwa asili hutokea wakati wa usiku na husababisha harufu mbaya kinywani wkati wa asubuhi, harufu huongezeka zaidi endapo utalala mdomo wazi. Tatizo sugu la mdomo kuwa mkavu huweza kusababishwa na matatizo ya uzalishwaji mate na baadhi ya magonjwa.
Madawa: Baadhi ya madawa huwa na harufu mbaya na mengine huchangia kusababisha kinywa kuwa kikavu.
Hata hivyo baadhi ya madawa baada ya kuvunjwa kwenye mfumo wa damu baadhi ya mazao ya uvunjwaji husafilishwa na kutolewa kwenye mapafu kama gesi na hili huchangia harufu mbaya kinywani.
Maambukizi katika kinywa: maambukizi katika vidonda vilivyo kinywani ama mdomoni huweza sababisha harufu mbaya kinywani, meno kuoza na magonjwa ya fizi huchangia pia kuleta harufu mbaya kinywani.
Matatizo mengine yam domo, pua na koo:tatizo la tonsil(kuvimba kwa tezi koo kutoka na maambukizi), maambukizi katika pua, uwazi katika kichwa na koo huchangia kutoa harufu mbaya kinywani.
Vitu vingine: sababu zingine kama, saratani kinywani na magonjwa kutokana kuharibika utendaji kazi ndani ya chembe hai husbabisha kutolewa kwa kemikali zinazosababisha harufu kinywani. Kupanda kwa aside tumbo kwenda kwenye koo huchangia kuleta harufu mbaya. Harufu mbaya kwa mtoto huweza kusababisha na kitu kigeni katika kinywa ama pua kilichooza kama vile chakula kilichokwama kwenye pua.
​
Soma zaidi makala nyingine kuhusu kinywa kutoka harufu mbaya kwa kubonyeza hapa
​
Imeboreshwa 3.07.2020