Kirusi cha Hepatiti B na Ini
Imeandikwa na madaktari wa ULY-CLinic
​
Maambukizi ya kirusi cha hepatitis B husababisha matatizo makubwa katika ini. Kwa baadhi ay watu ugonjwa huu huweza kuwa sugu ikimaanisha hudumu zaidi ya miezi sita. Kuwa na ugonjwa sugu wa kirusi huyu husababisha kufeli kwa ini kufanya kazi zake, saratani ya ini au kusinyaa kwa ini kutokana na makovu ya kudumu.
Watu wengi wanaopata maambukizi ya kirusi cha hepatitis B hupona, haka kama dalili na viashiria walivyopata vilikuwa vikali sana. Vichanga na watoto wadogo wanahatarishi ya kupata ugonjwa sugu. Chanjo ya kujikinga na kirusi huyu hutolewa kwa vichanga wanapozaliwa kwenye nchi nyingi ikiwemo Tanzania lakini cha kusikitisha hakuna tiba ya kuponya mara unapopata maambukizi. Kama umeambukizwa virusi hawa basi kuna hatua za kufanya ili kuzuia kueneza kwa watu wengine ugonjwa huu.
​
​
meboreshwa 7/11/2018