top of page

Maana

​

Visababishi

​

Vihatarishi

​

Dalili

​

Vipimo

​

Matibabu

Vipimo na utambuzi

​

Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic

​

Kama daktari atashuku kwamba una maambukizi ya kirusi cha hepatitis B, atakushauri au atakufanyia vipimo vya damu. Vipimo vya damu huweza kutambua kama unamaambukizi ya kirusi gani na maambukizi hayo ni sugu au ya mda mfupi. Kinyama kidogo kutoka kwenye ini kinaweza kuchukuliwa pia kwa ajili ya kufanyiwa kipimo kuona kama una uhalibifu kwenye ini lako. Sindano maalumu hupitishwa kwenye tumbo hadi kwenye ini na kuchukua kinyama hicho na kupelekwa maabara.

 

Kupimwa kwa watu wasioonyesha dalili

 

Madaktari wakati wmingine hupima watu wenye afya njema kipimo cha kutambua maambukizi haya kwenye damu zao kwa sababu kirusi anaweza kuharibu ini na kuleta dalili na viashiria baadae. Ongea na daktari wako kama

 

  • Unaishi na mtu mwenye maambukizi yakirusi cha hepatitis B

  • Ulifanya ngono na mtu menye maambukizi ya kirusi cha hepatitis B

  • Kemikali ini zako zinaonyesha kuwa zimepanda

  • Kama una maambukizi ya VVU au una maambukizi ya kirusi cha hepatitis C

  • Mgeni au umepata mtoto kwenye nchi zilizo na maambukizi ya juu ya kirusi huyu

  • Unatumia dawa za kulevya za kuchoma

  • Unafanya ushoga

  • Figo zako zimefeli na unachunjwa kwa kutumia mashine hospitali au kituoni(mashine za kuchangia)

  • Unakunywa dawa zinazoshusha kinga ya mwili

  • Una ujauzito

​

 

 

 

Imechapishwa 3/3/2015

Imeboreshwa 7/11/2018

bottom of page