Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
Visababishi
Homa ya hepatitis B hutokana na maambukizi ya kirusi cha hepatitis B. kirusi husafilishwa kati ya mtu mmoja na mwingine kwa njia ya damu, shahawa au majimaji ya mwili.
Njia kuu za usafilishaji huwa ni;
Tendo la kujamiiana- kama ukifanya ngono zembe, pasipo kutumia kinga ya kondomu, kufanya mapenzi na mtu aliyeambukizwa hukuweka hatarini mara 100 kupata homa ya kirusi huyu kupitia maji ya uke, mate, shahawa.
Kuchangia sindano-Kuchangia sindano na mtu aliyeathiriwa na kirusi huyu husababisha maambukizi kwako, kuchangia sindano za mishipa.
Kujichoma kwa bahati mbaya na sindano- kwa wale wafanyakazi wa afya njia hii huwa ni kuu katika kupata maambukizi ya kirusi huyu, pia watu wengine huweza kupata maambukizi haya endapo watachonwa na sindano za watu walio na kirusi huyu.
Mama kwenda kwa mtoto- kirusi huyu huweza kupita kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa. Hata hivyo kichanga anaweza kupewa chanjo ili kuzuia kupata maambukizi kwa vichanga vyote ongea na daktari wako kuhusu hali yako kama umeshapata maambukizi ya hepatitis B kabla ya kupata ujauzito ama unapokuwa mjamzito ili mpange kwa jinsi gani ya kumkinga mtoto.
Maambukizi ya mda mfupi na sugu
Maambukizi ya mda mfupi hutokea kwa watu wengi na hupona mapema zaidi kwa kipindi cha miezi michache, maambukizi ya mda mfupi yanaweza kuendelea kuwa sugu pia.
Maambukizi sugu ya hepatitis B
Hukaa miezi sita au zaidi. Kama mfumo wa kinga wa mwili wako hauwezi kupambana na maambukizi ya mda mfupi basi maambukizi haya huwa sugu na huweza kukaa maisha yako yote, na hivyo kupelekea matatizo makubwa kwenye ini kama kusinyaa na saratani vilevile.
Jinsi utakavyokuwa mdogo na kupata maambukizi haya haswa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano- hatarishi ya kupata ugonjwa sugu huongezeka. Maambukizi sugu yanaweza yasitambuliwe kwa karne kazaa mpaka mtu aumwe sana kutokana na ugonjwa mkubwa wa ini.
​
Imechapishwa 3/3/2015
imeboreshwa 7/11/2018