top of page

Homa baada ya kujifungua(kipindi cha puerperal)

 

Homa kipindi cha puerperal humaanisha kupanda kwa joto la mwili na kufikia kiasi cha degree 38C ama 100.4F (ambapo joto hili hupimwa mdomoni) katika vipimo viwili vya joto, kila kipimo kinafanyika masaa 24 baada ya kingine na mwanamke anakuwa ndani ya siku 10 toka siku ya kujifungua.

 

Nini husababisha homa hizi?

 

Mamboo mbalimbali yanaweza kuchangia kupata homa baada ya kujifungua ikiwa ni pamoja na;

 

  • Kusambaa kwa sumu za bakteria kwenye mfumo wa damu baada ya kujifungua,

  • Maambukizi ya UTI (kibofu, figo),

  • Maambukizi katika maziwa/titi,

  • Kuambukizwa kwa kidonda kilichotokana na kujifungua kwa njia ya upasuaji,

  • Maambukizi ya mapafu,

  • Maambukizi ya TB ya mapafu,

  • Ama homa iisiyo na sababu

​

imechapishwa 3/5/2015

Imeboreshwa 14/11/2018

Homa baada ya kujifunua
bottom of page