Imeandikwa na daktari wa ULY clinic
​
Dalili za Homa ya Ini
​
Utangulizi
​
Homa ya Ini ni ugonjwa unao sababishwa kwa asilimia kubwa na virusi vya hepataitiz, visababishi vingine vinaweza kuwa pamoja na magonjwa ya autoimnyuni, dawa, sumu kwenye damu na matumizi ya pombe.
​
Ugonjwa unatokeaje?
Maambukizi ya virusi vya hepataitiz hupelekea michomo kwenye ini kutokana na shambulio la virusi hao kwenye chembe za ini. Shambulio hili hupelekea kutokea kwa dalili mbalimbali ambazo zimeorodheshwa kwenye mada hii.
Hii kupelekea Ini kupata shida na kuvimba na kushindwa kufanya kazi vizuri. Hii hali huitwa Homa ya Ini au hepatitis.
​
Kuna Aina 5 ya Virus vya homa ya Ini na hivyo kuna aina 5 za hepataitiz inayosababishwa na virusi
-
Kirusi cha Hepataitiz A, husababisha Hepataitis A
-
Kirusi cha Hepataitiz B, husababisha Hepataitis B
-
Kirusi cha Hepataitiz C, husababisha Hepataitis C
-
Kirusi cha Hepataitiz D, husababisha Hepataitis D
Kirusi cha Hepataitis A na E
​
Huambukizwa kupitia chakula, maji ambayo hayako salama kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
​
Kirusi cha hepataitis na C
​
Huambukizwa kwa kupitia kugusa damu na majimaji mfano shahawa, majimaji ya ukeni kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
​
Dalili za ujumla za hepataitis
​
Zipo katika makundi (2) mawili
​
-
Dalili za muda mfupi
-
Dalili za kudumu
​
Dalili za muda mfupi
​
Dalili hizi za mwanzo hutokea ndani ya miezi 6 baada ya kuambukizwa virusi vya homa ya Ini, hutokea kwa baadhi ya watu hazitokei kwa kila mtu.
-
Uchovu wa mwili
-
Dalili za kutokwa na mafua
-
Kutoa haja kubwa iliyopauka
-
Mkojo mweusi kama soda ya koka kola
-
Kupoteza hamu ya kula
-
Kupungua uzito bila sababu ya msingi
-
Manjano kwenye Ngozi na macho​
-
Wakati mwingine manjano kwenye mate na mkojo
​
Dalili za kudumu
​
Dalili sugu huweza kutokea endapo mgonjwa hajapata tiba, badhi ya virusi huweza kuleta dalili sugu kama hepataitis A na B, dalili sugu hutokea endapo maambukizi ya virusi yamedumu kwa muda Zaidi ya miezi sita.
​
Baadhi ya dalili sugu ni;
-
Manjano endelevu
-
Kuvimba tumbo
-
Misuli kulegea
-
Mkojo uliopauka
-
Kuumia kirahisi na kutokwa na damu muda mrefu
-
Utokwa na damu bila sababu
-
Konfyusheni na
-
Kupungua uzito
-
kifo
​
​
Kumbuka chanjo dhidi ya hepataitis B inapatikana Hospitali, ni vema ukapata chanjo mapema.
​
​
Wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri endapo umeona una dalili hizi
​
​
Imeboreshwa 20.03.2020
​