Dalili
​
Imeandaliwa na madaktaro wa ULY-Clinic
​
Mara baada ya kungatwa na mbu aliyebeba vimelea wa plasmodium, mtu ambaye hana kinga huanza kuonyesha dalili baada ya siku saba au zaidi( siku 10-15)
Dalili za awali ni
-
Homa
-
Kichwa kuuma
-
Mwili kutetemeka
-
Kutapika
-
Dalili hizo zinaweza kuwa si kali kiasi kwamba ni vigumu kugundua ni malaria. Na endapo mtu asipotibiwa maambukizi ya baadhi ya vimelea wa malaria huendelea kuudhoofisha mwili na kuonesha dalili kali na kifo huweza kutokea.
Dalili zinazoonyesha malaria kali kwa mtoto ni hizi zifuatazo;
-
Upungufu mkali wa damu
-
Upumuaji wa shida
-
Malaria kupata kichwani- mtoto anaweza kuchanganyikiwa na kuongea vitu visivyoeleweka
-
Manjano
-
Mwili kulegea sana
Watu walio kwenye ukanda wa malaria hupata kinga ya mwili na hivyo huweza kutoonesha dalili endapo watangatwa na mbu wenye vimelea vya malaria.
imepitiwa 11/4/2016
imepitishwa 3/3/2015