Mwandishi:
Dkt. Benjamin M, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
22 Machi 2020 21:17:47
Kutunza kidonda cha upasuaji nyumbani
Sehemu hii utajifunza namna ya kutunza vidonda aina zote, vidonda vya upasuaji, na majeraha mengine.
Utunzaji wa vidonda, huhusisha mambo mawili kwanza kutunza kidonda na pili kupunguza maumivu yanayoweza kutokana na upasuaji au kidonda kutokana na jeraha.
Mbali na hivyo unatakiwa kujua dalili na ishara za hatari wakati unatunza kidonda zinazoweza kuashiria maambukizi kwenye kidonda ili kuzuia madhara yanayoweza kutokana na maambukizi hayo kwa kusafisha vema kidonda chako.
Ni vema pia kukumbuka vema maelekezo ambayo umepewa na daktari wako wakati unaruhusiwa kutoka hospitali. Unaweza kumuuliza mhudumu wako wa afya kukupa maelezo Zaidi kuhusu maelekezo ulopewa kama una shida kuyaelewa vema.
Aina za vidonda vya upasuaji
Kabla ya kujua namna ya kutunza kidonda ni lazima kujua aina za vidonda vinavyotokana na upasuaji;
Kuna aina 4 za vidonda ambavyo vinaweza kuhitaji upasuaji kurekebishwa
Kidonda kisafi
Huwa hakina dalili ya maambukizi au inflamesheni na havihitaji kuondolewa uchafu na hakitokani na kidonda kutokana na upasuaji wa kuondoa ogani ndani ya mwili. Vidonda hivi ni kama vile vidonda kutokana na upasuaji wa kwenye macho, Ngozi au mishipa ya damu. Hatari ya vidonda hivi kupata maambukizi ni chini ya asilimia 2
Vidonda visafi vilivyotiwa uchafu
hii ni aina ya kidonda ambacho hakina dalili ya maambukizi wakati wa upasuaji lakini huhusisha vidonda vya upasuaji wa kuondoa au kufanya marekebisho ya ogani ndani ya mwili. Mfano wa vidonda hivi ni vile vya upasuaji wa kwenye mapafu, apendeksi, na uke. Hatari ya kupata maambukizi ni asilimia 10
Kidonda kilichochanganyika na uchafu
Aina hii ya vidonda vinahusi vidonda vilivyo wazi vilivyotokana na ajali, vidonda cisafi vilivyotokana na ajali au kidonda kutokana na upasuaji wa kurekebisha au kundoa ogani ndani ya mwili na vidonda ambavyo damu au majimaji mengine yanaweza kumwagikia kwenye kidonda. Aina hii ya vidonda hatari ya maambukizi ni asilimia 13 hadi 20
Vidonda vichafu na vilivyochanganyika na uchafu
Vidonda hivi huwa vinamaambukizi wakati wa upasuaji. Hatari ya maambukizi ni asilimia 40
Madhumuni
Madhumuni ya kutunza kidonda baadaya upasuaji ni;
Kufanya kidonda kipone haraka bila maambukizi
Kufanya eneo lenye kidonda lijirudie vizuri karibia na mwonekano wake wa mwanzo
Utunzaji wa kidonda cha upasuaji
Ni vema ukamuuliza daktari wako namna ya kusafisha na kutunza kidonda chako. Kama una kidonda kilichofungwa baada ya kufanyiwa upasuaji msafi, kidonda kinaweza kujifunga chenyewendani ya masaa 24 hadi 48. Unaweza kuondoa bandaji na kuoga kama ulivyoelekezwa na daktari wako.
​
Haya ni baadhiya maelekezo ya ujumla ya kutunza kidonda chako.
Tumia maji ya bomba au shawa wakati wa kuosha kidonda
Zuia kuoga kwenye jokofu, swimming pool na maji ya moto mpaka kidonda kimepona
Vivywalo vya kidonda vinaweza kuumiza kidonda wakati wa kutoa, vitatakiwa kuloanishwa kabla ya kuvitoa
Usitumie dawa za antiseptiki au disinfektanti kama hydrogen peroxide, spiriti au iodine kuosha kidonda kilicho wazi. Kemikali hizi hubomoa kidonda badala ya kufanya kipone
Kutumia gozi kwenye kidonda kunaweza kusababisha maumivu, matumizi ya vivyalo maalumu kwa ajili ya kidonda kama hydrogels, hydrofibres, alginates na silicone laini huzuia maumivu kwa asilimia nyingi
Maumivu ya kidonda yanaweza kuzuiliwa kwa kutumia dawa za kununua duka la dawa baridi au kuandikiwa na daktari wako
Kusafisha kidonda cha upasuaji
Ni muhimu kufuata maelekezo ya daktari ya namna ya kuosha kidonda chako. Aya inayofuata chini imeelezea namna ya kuondoa gozi kwenye kidonda kabla ya kuoga au kusafisha kidonda
Kama mikono yako inaonekana kuwa na uchafu, tumia sabuni na maji kunawa mikono kwa muda wa sekunde 10 hadi 30. Endapo mikono yako haionekani kuwa na uchafu unaweza kutumia Mafuta ya kusafishia mikono yenye spiriti asilimia 60.
Baada ya mikono kuwa misafi, legeza gozi kidogo, usiiondoe yote kwa hatua hii
Vaa glavu za tiba au tumia karatasi ya plastiki kuondolea gozi kwenye kidonda. Tupa uchafu wote kwenye kwenye ndoo ya kutunzia uchafu
Osha mikono yako tena au tumia tena Mafuta ya kusafisha mikono yenye spiriti asilimia 60
Kuosha kidonda cha upasuaji wakati usio wa kuoga
Kama mikono yako inaonekana kuwa na uchafu, tumia sabuni na maji kunawa mikono kwa muda wa
sekunde 10 hadi 30. Endapo mikono yako haionekani kuwa na uchafu unaweza kutumia Mafuta ya
kusafishia mikono yenye spiriti asilimia 60.
Chovya gozi safi kwenye maji ya bomba au kutumia maji maalumu ya kununua duka la dawa kama
unayo au umeambiwa kuyatumia
Eneo ambalo limeshonwa au kubanwa na stepla ni eneo ambalo huwa na uchafu kiasi, hili linatakiwa
kuwa la kwanza kusafishwa na kicha eneo la nje linafuatia. Usirudi tena katikati ya kidonda wakati wa
kusafisha kwa kutumia gozi ile ile kuzuia kuleta uchafu. Siku zote anza na katikati kwenda nje.
Tembeza gozi iliyochovywa kwenye maji taratibu kuzunguka eneo la kidonda kilichoshonwa kwa nyuzi
au kutumia steri strips ili kusafisha na kuondoa damu iliyokauka au majimaji yanayotoka kwenye kidonda cha upasuaji.
Rudia hizi mara nyingine na kisha kikaushe kidonda kwa gozi kavu au taulo safi
Kusafisha kidonda wakati unaoga
Fuata hatua zifuatazo kusafisha kidonda cha upasuaji wakati unaoga kwa ya bomba la mvua
Tumia kiti kukaa kwa utulivu, rekebisha maji ya mvua yaanze kutoa maji yenye uvuguvugu kiasi na yasitoke kwa kasi kuzuia kutenganisha au kuumiza kidonda. Maji yasiwe ya moto.
Acha maji ya shawa yatiririke kwenye kidonda kwa dakika 5 hadi 10, hakikisha kidonda kinakaa mbali na bomba la shawa ili kisigusane na shawa.
Mambo ya kuzingatia
Mambo muhimu ya kuzingatia unapokuwa unasafisha kidonda cha upasuaji
Hakikisha hutumii nguvu kusafisha kidonda ili kuzuia kidonda kufunguka au nyuzi kuachia
Nawa mikono kala ya kusafisha kidonda
Kama kidonda cha lasalesheni kipo juu ya kichwa, unaweza kutumia sabuni ya shampuu kuosha nywele za juu ya kichwa. Tumia nguvu kidogo na zuia maji yasitiririke kwa nguvu sana kwenye kidonda
Mpigie daktari wako kama una maswali Zaidi kuhusu namna gani ya kusafisha kidonda chako na namna gani ya kutunza nyuzi za kidonda
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
21 Julai 2023 16:20:09
Rejea za mada hii;
1. Surgical site infections. John Hopkins University.
www.hopkinsmedicine.org/healthlibrary/conditions/surgical_care_site_infections_134,144. Imechukuliwa
mwezi machi 22.2020
2. Weller R, Hunter H, Mann MW. Clinical dermatology. Toleo la 5. Hoboken, NJ:Wiley-Blackwell;
Imechukuliwa mach 22.2020.
3. Sarvis C. Postoperative Wound care. Nursing 2006. 2006; 36(12):56-57
4. U.S. Department of Jealth and Human Services. Agency for Healthcare, Research and Quality (AHRQ).
Surgical site infection: prevention and treatment of surgical site infection
www.guidline.gov/content.aspx?id=13416. Imechukuliwa mach 22.2020
5. National Instituete for health and Care Excellence (NICE)
6. Surgical site infections: prevention and treatment. October 2008;
www.nice.org.uk/guidence/cg74. Imechukuliwa machi 22.2020 murphy PS, Evans GR. Advances in
wound Hearing: A review of current wound hraling products. Plast surg Int. 2012;2012:190436. Doi:
10.1155/2012/190436.Epub2012 March 22.
7. Walter CJ, Dumville JC, sharp CA, Page T.Systemic review and meta-analysisof wound dressing in the
prevention of surgical site infections in surgical wounds healing by primary intention. Br J Surg.
2012;99:99:1185-1194.
8. Timmons J, Gray D, Russell F. Silflex soft silicone wound contact dressing. Wounds UK; 2009;5(2):56-61
9. Upton D, Stephens, AndrewsA. Patients experience of negative pressure wound therapy for the
treatment of wounds: areview. J Wound care. 2013 jan;22(1): 34 39.DOI.ORG/10.12968/jwc.2013.22.1.34