top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

26 Machi 2021 09:47:46

Matibabu ya maumivu ya koo

Matibabu ya maumivu ya koo

Maumivu ya koo ni dalili ya hisia za kuhisi maumivu, ukavu au kukwanguliwa kwa koo. Tatizo hili huwapata watu wengi duniani.


Mara nyingi maumivu ya koo husababishwa na maambukizi ya virusi na hewa kavu kwenye mazingira na mara nyingi dalili hii hupotea yenyewe bila matibabu.


Aina za maumivu ya koo


Kuna aina tatu za maumivu ya koo kulingana na sehemu ya koo iliyoathiriwa, ambazo ni


Uvimbe wa koromeo (pharynx)

Uvimbe wa findo ( tonsils)

Uvimbe wa zoloto (larynx)


Vishiria vya maumivu ya koo


Viashiria vya maumivu ya koo ni pamoja na;


  • Hisia za kukwanguliwa koo

  • Hisia za kuungua koo

  • Kukauka kwa koo

  • Kukereketa kwa koo

  • Maumivu ya koo likishikwa

  • Kuonekana kwa usaha au mabaka meupe kwenye koo


Matibabu ya nyumbani ya maumivu ya koo


Visababishi vingi vya maumivu ya koo vinaweza kutibiwa nyumbani. Matibabu ya nyumbani ya maumivu ya koo huhusisha;


  • Kupata muda wa kupumzika ili kuupa mwili wako muda wa kupambana na maambukizi

  • Sukutua kinywa kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye chumvi kijiko kimoja kwa kila kikombe kimoja cha chai au robo rita ya maji

  • Kunywa maji au vinywaji vya uvuguvugu vinavyokupa nafuu kwenye koo kama vile chai ya moto yenye asali, supu au maji ya moto yenye limao

  • Pooza koo lako kwa kutumia vitu vya baridi kama vile kula barafu. Baadhi ya watu hawafai kutumia barafu kwa sababu huamsha tonses.

  • Tumia kiyoyozi ili kuongeza hewa ya unyevu kwenye mazingira endapo kuna hewa kavu ndani

  • Endapo wewe ni mwimbaji au muongeaji sana, pumzisha koo lako mpaka utakapokuwa vema


Tiba ya maumivu ya koo kwa kutumia magadi soda


Unatakiwa kuwa na unga wa magadi soda yaliyochomwa moto, limao moja na asali mbichi ya nyuki wadogo kama inapatikana au asali ya nyuki wakubwa, kikombe kimoja tupu na kijiko cha chai.


Namna ya kuchanganya magadi soda, asali na limao kutibu maumivu ya koo


1. Kwa kutumia vidole chota kiasi kidogo ( takribani moja ya nane ya kijiko cha chai) tu cha unga wa magadi


Kisha

2. Weka kwenye kikombe tupu


Kisha

3. Kamulia maji ya limao au ndimu moja kubwa, kisha utaona povu likitengenezwa na baada ya povu kuisha

4. Weka vijiko viwili vya asali kwenye mchanganyiko huo


Kisha

5. Changanya kwa kijiko mchanganyiko wako.

6. Baada ya kupata mchanganyiko huo kunywa. Unaweza kufanya hivi mara mbili kwa siku kwa muda wa siku mbili tu.


Matibabu mengine ya nyumbani huhusisha

  • Kutumia chai ya tangawizi kwa wingi

  • Kutumia chai iliyokamuliwa ndimu pamoja na kuweka asali

  • Kutumia chai ya maua ya chamomile

  • Kufanya sauna


Kumbuka.


Shauriana na daktari wako siku zote kabla ya kutumia matibabu haya ili achunguze na kuona kama inafaa kwako.


Maelezo ya ziada kuhusu matibabu ya maumivu ya koo


Pata maelezo ya ziada kuhusu maumivu ya koo kwa kutafuta kwenye boksi la tafuta chochote hapa juu ya tovuti hii. Andika neno 'maumivu ya koo' kisha tafuta na kusoma.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:18:21

Rejea za mada hii;

1. Herbal tea helps reduce the pain of acute pharyngitis. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC200788/. Imechukuliwa 26.03.2021

2. Josef Brinckmann, et al. Safety and efficacy of a traditional herbal medicine (Throat Coat) in symptomatic temporary relief of pain in patients with acute pharyngitis: a multicenter, prospective, randomized, double-blinded, placebo-controlled study. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/12804082. Imechukuliwa 26.03.2021

3. Andrew B Jull, et al . Honey as a topical treatment for wounds. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23450557. Imechukuliwa 26.03.2021

4. https://www.cancer.gov/publications/patient-education/mouth-and-throat.pdf. Imechukuliwa 26.03.2021

5. Carol S. Johnston, et al. Vinegar: Medicinal Uses and Antiglycemic Effect. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1785201/. Imechukuliwa 26.03.2021

6. P Josling . Preventing the common cold with a garlic supplement: a double-blind, placebo-controlled survey. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/11697022/. Imechukuliwa 26.03.2021

7. Mohammad Hassan Emamia, eta al. Respiratory Tract Infections and its Preventive Measures among Hajj Pilgrims, 2010: A Nested Case Control Study. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3793484/. Imechukuliwa 26.03.2021

bottom of page