Matibabu ya Nyumbani
Sehemu hii utajifunza namna ya kumuhudumia mgonjwa au ya kujihudumia mwenyewe ukiwa nyumbani. Utahitaji msaada kidogo wa maelekezo kutoka kwa daktari wako au daktari wa
ULY CLINIC
Kutoa mdudu sikioni
Mdudu kuingia masikioni ni jambo linaloweza kutokea kwa kila mtu. Muda muafaka huweza kuwa wakati umekaa mchana au wakati umelala usiku. Wadudu wanaoweza kuingia sikioni ni mbu, nzi, mende na wengine. Mdudu anaweza kuingia sikioni na akaishi muda mrefu au akafia ndani bila wewe kufahamu.
Kutokwa na damu puani matibabu
Kutokwa na damu ndani ya pua kwa lugha tiba huitwa epistaksizi, huweza kutokea kipindi cha ujana au utotoni kwenye umri fulani. Tatizo hili husababisha hofu kwa mzazi au mtoto, hata hivyo huna haja ya kuogopa kwa sababu tatizo hili mara nyingi huwa si hatari na karibia kila mtu ashapata mara moja katika maisha yake.
Matibabu ya presha pasipo dawa
Kuna njia nyingi unaweza tumia kushusha shinikizo la damu endapo hutaki tumia dawa;
Kwa kula vyakula vyenye mboga za majani kwa wingi, matunda na mbegu. Fuata ushauri wa mlo maalumu kama ilivyoelezewa katika makala hii. Kumbuka kwenye makala hii imeelezewa taarifa za awali tu, taarifa zaidi zinapatikana kwa madaktari wa ULY CLINIC.