top of page
Matibabu ya Nyumbani
Sehemu hii utajifunza namna ya kumuhudumia mgonjwa au ya kujihudumia mwenyewe ukiwa nyumbani. Utahitaji msaada kidogo wa maelekezo kutoka kwa daktari wako au daktari wa
ULY CLINIC

Muda wa kutoa nyuzi za upasuaji
Nyuzi za kidonda, ni nyuzi laini zinazoshonwa kwenye kidonda ili kukutanisha kuta za kidonda ili kiweze kupona. Nyuzi zinaweza kuwa za kuyeyuka au zisizo za kuyeyuka, nyuzi za kuyeyuka mara nyingi huyeyuka ndani ya wiki 4 hadi 8. Nyuzi za kuyeyuka huwa hazihitaji kutolewa kwenye kidonda kwa kuwa huyeyuka zenyewe.
bottom of page