Kurasa hii imeorodhesha homon mbalimbali zinazopatikana kwenye mwili wa binadamu
Estrone
Estrone ni homoni inayozalishwa na ovari ,ni moja ya homoni yenye umuhimu sana kwa mwanamke bada ya komahedhi. Estron ipo kwenye kundi la homoni za oestrogens ambazo zipo nne estrone (E1), estradiol (E2), estriol (E3), and estetrol (E4 ).
Norepinephrine ni homoni inayojulikana kwa jina jingine la noradrenaline, homoni hii hufanya kazi kama homoni na nyurotransmita (mjumbe) wa kusafirisha taarifa za mfumo wa fahamu kati ya neva moja na nyingine.
Homoni ya melatonin hufahamika kwa jina jingine la N-acetyl-5-methoxytryptamine huwa na rangi ya blue na hutengenezwa kutoka kwenye amino asidi zinazoitwa tryptophan. Homoni hii hufahamika kama homoni ya usingizi