top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Alhamisi, 16 Aprili 2020

Cholecystokinin

Cholecystokinin

Utangulizi

Kolesaitokainini (Cholecystokinin) (CCK) ni homoni ambayo Hujulikana kama pankriozaimini inayopatikana kwenye mfumo wa gastrointestino. Homoni hii inahusika na umeng’enyaji wa chakula na pia huwa na kazi zingine kama Kiasi kuthibiti woga , wasiwasi na hali ya huzuni.

Homoni hii huzalishwa baada tu ya mtu kula chakula ili kufanya umeng’enyaji wa chakula, kuruhusu kifuko cha nyongo kutoa nyongo kwa ajili ya umeng’enyaji wa chakula chenye Mafuta, wang ana protini na kupunguza hamu ya kula(kuuambia mwili kuwa tumbo limejaa) mara baada ya tumbo kupata chakula.

Homoni hii huzalishwa na Seli I zilizo kwenye utumbo wa duodenamu, na pia huzalishwa na baadhi ya neva zilizo kwenye ubongo.

Hufanya kazi kupitia risepta mbili katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na ubongo.

Kazi zake kuu ni umeng’enyaji wa chakula na kusababisha mwili uone umeshiba baada ya kula.

Hutumika kumfanya mtu kuhisi kuwa ameshiba baada ya kula na kumpunguzia hamu ya kula

Jinsi gani homoni hii huweza kuthibitiwa?

Kuingia kwa chakula chenye Mafuta nap rotini tumboni huamsha uzalishaji wa homoni ya kolesaitokainini dakika 15 baada ya kula na hubakia kuwa kwenye damu kwamuda wa masaa matatu.

Uzalishwaji huu hudhibitiwa na homoni nyingine ya mfumo wa gastrointestino inayojulikana kwa jina la somatostatin. Hata hivyo uzalishwaji pia huweza dhibitiwa na tindikali na asidi ya nyongo iliyotolewa kwenda kwenye utumbo baada ya kula chakula.

Tafiti zinaonyesha hakuna mgonjwa amewahi kufahamika kuwa na tatizo la uzalishwaji kwa wingi wa homoni hii, hata hivyo watengeneza dawa za kupunguza uzito wamejaribu kuiga namna homoni hii inavyofanya kazi ili kusaidia kupunguza uzito.

Tafiti zinaonyesha watu wanene wana kiasi kidogo cha homoni ya kolesaitokainini na hivyo hujiona kuwa hawajashiba na kula Zaidi.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

16 Aprili 2020 09:48:43

Rejea za mada hii;

bottom of page