top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Ijumaa, 17 Aprili 2020

Estriol

Estriol

Utangulizi

Ni moja kati ya homoni nne za estrogen yaani estriol, estradiol, estrone, na estetrol. Homoni hii hujulikana kwa jina jingine la Oestriol au E3

Estriol ni moja ya homoni zinazozalishwa kwa wingi wakati wa ujauzito . homoni ya estrol ni homoni dhaifu ukilinganisha na homoni zingine za estrogen, huzalishwa na huzalishwa na ukuta wa sin-sishotrophoblasti. Ukuta huu ufanyika mara baada ya uchavushwaji wa yai la kike na huwa na hutengeneza kichanga tumboni.

Kiwango cha homoni ya estriol kwenye damu huanza kuongezeka kuanzia wiki ya 8 hadi 9 ya ujauzito na hushuka wakati mama anaelekea kujifungua.

Jinsi inavyozalishwa;

Hutengenezwa na kondo la nyumala ujauzito, utengenezaji pia hutegemea ushirikiano baina ya Ini na figo ya mtoto. Ukamilishaji wa uzalishaji wa homoni ya estriol hufanywa na Kondo la nyuma(plasenta).

Kazi za Estriol

• Humuandaa mama kwa ajili ya leba na kunyonyesha
• Kiwango cha homoni ya estriol kwenye damu kinatumika kutambua hali ya kiafya ya mtoto tumboni mwa mama, kiwango kikiwa kidogo kinaweza kumaanisha mtoto anashida.
• Hutumika kutambua matatizo ya kimaumbile ya mtoto akiwa tumboni.
• Estriol huimarisha mfuko wa uzazi kwa ajili ya ukuaji wa mtoto na badae huandaa mwili kwa ajili ya kujifungua
• Huongeza ute ute kwenye uke, hivyo huzuia uke kuw amkavu

Kuzidi kwa homoni ya Estriol;

Endapo kiwango cha Homoni ya estriol kitazidi kwenye damu huwa ni ishara mama atajifungua kabla ya wakati (kupata mtoto njiti) au (leba) uchungu unakaribia.

Uchache wa homoni ya Estriol;

Kiwango cha chini kisicho cha kawaida wkenye damu cha homoni ya estriol humaanisha kuna shida ya kimaumbile ya mtoto mfano tatizo la Down syndrome au tatizo kwenye plasenta.

Kiwango cha chini cha homoni hii karibia na kipindi cha kujifungua huweza kuashiria kuwa mama atachelewa kujifungua na hivyo atahitaji njia nyingine za kuanzisha na kuchochea uchungu(leba)


Kuna dawa ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kutibu matatizo yanayoambatana na upungufu wa homoni hii. Dawa ya homoni mbadala ya estriol hutumika kutibu matatizo yanayotokana na komahedhi. Dawa hizi pia hupunguza hali ya mifupa kuvunjika kirahisi kwa kuifanya iwe imara kwa wanawake walio kipindi cha komahedhi.

Baadhi ya maudhi madomadogo ya dawa za homoni mbadala ya estriol pamoja na tumbo kujaa gesi, vipele kwenye matiti ,maumivu ya kichwa, kubana kwa misuli ya miguu, kutokwa na damu kwenye ukeni na kichefuchefu.

Kula mboga za majani ,matunda na mboga jamii ya kunde huweza kusaidia katika kuchochea uzalishwaji wa homoni ya estriol.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

17 Aprili 2020 08:33:56

Rejea za mada hii;

bottom of page