top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Alhamisi, 9 Aprili 2020

Glucagon

Glucagon

Utangulizi

Ni homoni inayozalishwa na tezi ya kongosha, katika seli zinazoitwa alpha. Hufanya kazi pamoja na homoni zingine mwilini ili kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

Homoni hii hufanya kazi ya kuongeza kiwango cha glukosi na mafuta ya fati aside kwenye damu.

Je glucagon hutolewa wakati gani?

Glucagon hutolewa pale ambapo sukari katika damu inapokuwa ndogo na katika matukio ambayo mwili unahitaji sukari ya kutosha mfano wakati wa kukutana na tukio la ghafla au wakati wa kazi ngumu.

Glucagon inapotolewa hufanya kazi zifuatazo:

• Huchochea Ini kuvunja glycogen kuwa glukosi
• Huchochea glukoneojenesisi (kubadilishwa kwa amino asidi kuwa kuwa glukosi)
• Kuvunja vunja mafuta ya fati asidi iliyohifadhiwa kuwa chanzo cha nishati mwilini.

Glukagon hufanya kazi ya kuhakikisha kiasi cha glukosi kwenye damu kipo sawa na kuhakikisha kuwa shughuli zote za mwili zinaendelea kwa kupata glukosi.

Kiwango cha glucagon kwenye damu hupungu apale mtu anapokula vyakula vyenye sukari kwa wingi, na hupanda pale mtu anapokula vyakula visivyo na sukari ili kusaidia mwili ujitengenezee sukari ya glukosi
Kwa mgonjwa wa kisukari, kiwango cha glucagon mwilini mwake huwa chini.

Uhusiano wa Glucagon na Insulin katika utendaji kazi ukoje?

Mara tu chakula cha wanga kinapoingia mwilini , vimeng'enya mbalimbali vya wanga hubadilisha wanga ili kuwa sukari ya glukosi kisha hufyonzwa na kusafirishwa kwenye damu.

Kiwango cha glukosi kinapopanda kwenye damu, tezi ya kongosho hutoa homoni ya Insulin inayofanya kazi ya kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Kiwango cha glukosi kikizidi, insulin hubadili glukosi kuwa glycogeni na kuihifadhi kwenye Ini

Kiwango cha glukosi kinapokuwa chini ya kiwango kwenye damu, kongosho pia hutoa homoni ya glukagoni ili kubadilisha glaikojeni kuwa glukosi, hivyo kuongeza kiwango cha sukari kwenye damu.

Mtu anapokuwa na kiwango cha chini cha homoni ya glucagon huweza kuwa na dalili za;

• Njaa
• Kutetemeka
• Kuwa na woga na wasiwasi
• Kuchoka
• Kutokwa na jasho sana
• Ngozi kuwa nyeupe
• Kulala sana
• Kizunguzungu

Mtu mwenye kiwango cha juu cha homoni ya glukagoni huwa na dalili za;

• Kuwa na kiu ya maji mara kwa mara
• Maumivu ya kichwa
• Kutokuona vizuri
• Kukojoa mara kwa mara
• Kuchoka na kuwa mdhaifu
• Kupungua uzito


Matibabu ya mtu mwenye upungufu wa glucagon

Mtu anaweza kupata dawa za kutumia ili kuongeza kiwango cha homoni ya glukagoni kwenye damu.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

9 Aprili 2020 10:55:49

Rejea za mada hii;

bottom of page