top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Jumapili, 5 Aprili 2020

Oxytocin

Oxytocin

Oxytocin ni homoni muhimu mwilini haswa kwa wanawake, huzalishwa katika tezi ya haipothalamasi na kuhifadhiwa sehemu ya nyuma ya tezi ya pituitari. Endapo mwili unahitaji kutumia homoni hii pituitari huitoa kwenye mishipa ya damu ili isafirishwe na kufika eneo ambapo inahitajika. Homoni hii hufanya kazi kama homoni na nurotransmita.

Kazi kubwa mbili ya homoni oxytocin ni kuongeza mijongeo(uchungu) ya tumbo la uzazi wakati wa kujifungua na uzazlishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Homoni hii hushinikiza misuli ya kizazi ijongee ili kumtoa mtoto tumboni, pia huongeza uzazlishaji wa prostaglandini. Kuongezeka kwa prostagalndini huongeza Zaidi uchungu wa uzazi.

Homoni hii hupatikana kama dawa, dawa hii hutumika hospitali kuongeza uchungu wa uzazi, kuharakisha kujifungua kwa wamama walio kwenye uchungu na kuanzisha uchungu kwa wamama wasio na uchungu lakini wakati wa kujifungua umefika.

Mara baada ya kujifungua, homoni ya oxytocin huchochea utoaji wa maziwa ya mama yaingie kwenye titin a kutolewa katika chuchu.

Homoni hii kwa wanaume huwa na kazi pia za kujongeza manii na kuongeza uzazlishaji wa homoni testosterone kutoka kwenye korodani.

Tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mbali na kazi zilizotajwa hapo juu, husaidia kumrekebisha mtu kwenye mambo ya kijamii mfano, kuhamasisha hisia za kujamiana, kupenda, furaha, kutambua, uaminifu, shauku na kuongeza muungano wa mama na kichanga wake. Hivyo kwa jina jingine huitwa kama homoni ya upendo. Homoni zingine zinazofanya kazi ya upendo kama oxytocin ni dopamine, endorphin na serotonin.

Uzalishaji wa homoni hii hudhibitiwa kwa njia ya mrejesho chanya, mara kiwango cha homoni kimapoongezeka kwenye damu, taarifa hutumwa kwenye ubongo na ubongo huongeza uzazlishaji Zaidi wa homoni ili kuongeza uvhungu Zaidi.

Mara mtoto anapozaliwa homoni hii hupungua kwenye dam una kwua kiwango cha kawaida. Hata hivyo mtoto anapokuwa ananyonya homoni hii huzalishwa ili kuongeza utoaji wa maziwa. Kiwango huongezeka zaidi mtoto anapokuwa ananyonya, mara mtoto atakapoacha kunyonya kiwango cha homoni hurejea kuwa cha kawaida. Mtoto atakapoachishwa kunyonya homoni hii hupungua kwenye dam una uzalishaji wa maziwa unasimama.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

5 Aprili 2020 13:57:34

Rejea za mada hii;

bottom of page