Imeandikwa na daktari wa ULYclinic
Alhamisi, 16 Aprili 2020
Calcitonin
Utangulizi
Kalsitonini (Calcitonin) ni homoni inayozalishwa na seli C za tezi ya thairoidi, Homoni hii huwa na kazi kuu ya kuthibiti kiasi cha madini ya Calcium na phosphate kwenye damu na kusimamisha utendaji wa homoni ya parathairoidi.
Homoni ya kalsitonini hutumika kuthibiti kiasi cha wingi wa kalisiamu kwenye damu kwa njia kuu mbili;
• Huzuia shughuli za seli zinazohusika na uvunjwaji wa seli za mifupa (osteoklasti) ,hii ni kwa sababu seli hizi zinapovunjwa huachilia madini ya kalisiamu kwenye mkondo wa damu ,hivyo kuzuia kuvinjwa kwa seli za mifupa na homoni hii husababisha kuthibiti kiwango cha madini ya kalisiamu kwenye damu kwa muda mfupi.
• Huruhusu figo kupoteza madini ya kalisimu kwenye mkojo.
Uzalishaji wa Homoni ya kalsitonini hudhibitiwaje?
Uzalishaji wa homoni ya kalsitonini hutegemea kiasi cha madini ya kalisiamu kwenye damu
Kiwango cha madini haya kinapozidi kiwango cha kawaida kwenye damu, homoni ya Kalsitonini hutolewa kwa wingi
Kiasi cha madini ya kalisiamu kinapopungua kwenye damu, homoni ya kalsitonini nayo hupungua.
Hata hivyo uzalishaji wa homoni hii huweza kudhbitiwa na homoni ya utolewaji somatostatini ambayo pia hutolewa na seli C za tezi ya thairoidi
Kuzidi kwa homoni ya kalsitonini kwenye damu kunaweza kusababishwa na saratani yay a seli C za tezi ya thairoid
Kupungua kwa homoni ya Kalsitonini hakuambatani na madhara yeyote katika mwili, hii ni kutokana na wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kuondolewa tezi ya thairoidi kutoonyesha dalili zozote za upungufu wa homoni hii.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
16 Aprili 2020 09:20:09
Rejea za mada hii;
- 1.YourHormone.Calcitonin.https://www.yourhormones.info/hormones/calcitonin/. Imechukuliwa 15/4/2020
2.Hormone.Calcitonin.https://www.hormone.org/your-health-and-hormones/glands-and-hormones-a-to-z/hormones/calcitonin. Imechukuliwa 15/4/2020
3.Britannica.calcitoni.https://www.britannica.com/science/calcitonin-hormone. Imechukuliwa 15/4/2020
4.ScienceDirect.Calcitonin.https://www.sciencedirect.com/topics/pharmacology-toxicology-and-pharmaceutical-science/calcitonin. Imechukuliwa 15/4/2020