top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Alhamisi, 16 Aprili 2020

Erythropoietin

Erythropoietin

Utangulizi

Erythropoietin (Erithropoietini) ni homoni inayozalishwa na figo kwa asilimia 90 na kwa kiasi kidogo sana huzalishwa na Ini, homoni hii huwa na kazi kuu ya kuchochea urojo wa mifupa(bone marrow) kuzalisha chembechembe nyekundu za damu.

Homoni hii huwa pungufu mwilini kwenye baadhi ya magonjwa sugu kama magonjwa ya figo na UKIMWI, wanasayansi wametengeneza homoni hii maabara na inawez akutumika kama dawa kwa wagonjwa wenye upungufu wa homoni.

Homoni hii huzalishwa na figo endapo damu inayopita kwenye mishipa ya figo ina kiwango kidogo cha hewa ya oxksigen. Kushuka kwa kwango cha oksijeni kwenye damu huambatana na kiwango kidogo cha chembe nyekundu za damu, hivyo figo hutoa homoni ili kuzalisha chembe nyekundu za damu.

Kazi kubwa za Erithropoietini ni;

• Kuchochea utengenezwaji wa chembe nyekundu za damu
• Huchochea utengenezwaji wa himoglobini ambayo hufanya kazi ya kubeba oksijeni ndani ya chembe nyekundi ya damu.

Sababu zinazoweza kupelekea kupungua kwa homoni ya erithropoietini ni magonjwa sugu ya figo, na sababu zinazoweza kupelekea kuzidi kwa kiwango cha homoni hii kwenye damu ni baadhi ya saratani kwenye figo.

Magonjwa yanayotokana na kuzidi kwa homoni hii ni ugonjwa wa polysaithemia vera unaotokana na kuzidi kwa chembe nyekundu za damu mwilini ambapo mara nyingi hakuna dalili. Kama dalili zitatokea ni Pamoja uchovu wamwili, maumivu ya kichwa, kuwashwa, maumivu ya jointi na kizunguzungu

Magonjwa yanayotokana na upungufu wa homoni hii ni upungufu wa damu mwilini(anemia). Baadhi ya dalili za anemia ni Pamoja na uchovu wa mwili, manjano kwenye Ngozi, mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo, kuishiwa pumzi, kizunguzungu na maumivu ya kichwa, kuhisi baridi kwenye miguu na mikono na maumivu ya kifua

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

16 Aprili 2020 11:34:00

Rejea za mada hii;

bottom of page