top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Ijumaa, 17 Aprili 2020

Glucagon like peptide-1 (GLP-1)

Glucagon like peptide-1 (GLP-1)

Utangulizi

Homoni ya glukagoni inayofayofanana na peptaidi (Glucagon like peptide 1) ni homoni inayozalishwa kwenye mfumo wa gastrointestino kufuatia mwitikio wa chakula kinacho ingia tumboni, hujulikana kwa jina jingine la incretin.

Homoni hii inayozalishwa na seli L za Gastrointestino, huwa na kazi ya kupunguza hamu ya kula (kwa kuleta hisia za kushiba baada ya chakula kuingia tumboni) na huchochea kuzalishwa kwa homoni ya insulin.

Uchocheaji uzalishaji wa homoni ya insulin hufanyika kwa kuongeza utoaji wa homoni na kuongeza seli za kuzalisha insulin kwenye tezi ya kongosho. Mbali n ahivyo homoni hii huchochea uzalishaji wa homoni ya glucagon.

Hata hivyo kongosho na mishipa ya fahamu pia huwa inazalisha kwa kaisi kidogo homoni ya glucagon like peptide 1 (GLP-1)

Mara baada ya kula homoni hii hutuma taarifa kwenye ubongo kupitia mishipa ya fahamu kwamba kiasi cha chakula unachokula kinatosha hivyo kufanya uhisi umeshiba.

Jinsi gani huweza kuthibitiwa;

Mara chakula kinapoingia tumboni, uzalishwaji wa homoni huanza kufanyika, ndani ya dakika 10 kiwango cha homoni hii huongezeka mara dufu kwenye damu na kufanza kufanya kazi yake. Homoni inapotolewa kwenye damu huweza kudhumu kwa muda wa masaa kadhaa kabla ya kiwango chake kurejea kile cha asili kwenye damu.

Pia uzalishwaji wa homoni ya GLP-1 hudhibitiwa na homoni ya somatostatin inayozalishwa pia kwenye mfumo wa gastrointedtino(soma zaidi kuhusu homoni ya somatostatin sehemu nyingine kwenye Makala zetu).
Hakuna mgonjwa aliyeripotiwa kuwa na kiwango kikubwa kuliko cha kawaida cha homoni hii. Wanasayansi wamekuwa wakijaribu kuiga namna ya homoni hii inavyofanya kazi ili kutengeneza dawa ya kisukari aina ya 2.

Upungufu wa uzalishwaji wa homoni hii hupelekea mtu kula sana kwa sababu ya kutohisi hali ya kushiba anapokuwa anakula. Matatizo ya uzito mkubwa na obeziti huweza kutokea kwa watu hawa.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

17 Aprili 2020 07:36:08

Rejea za mada hii;

bottom of page