top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Ijumaa, 17 Aprili 2020

Melatonin

Melatonin

Utangulizi

Melatonin ni homoni inayozalishwa mwilini na tezi pinio(pineal), tezi hii ni ndogo sana yenye umbo la kunde hupatikana kwenye ubongo.

Homoni ya melatonin hufahamika kwa jina jingine la N-acetyl-5-methoxytryptamine huwa na rangi ya blue na hutengenezwa kutoka kwenye amino asidi zinazoitwa tryptophan. Homoni hii hufahamika kama homoni ya usingizi.

Melatonin huwa na kazi kubwa ya kurekebisha mzunguko mzima wa kulala na kuamka. Uzalishaji wa homoni ya melatonin kwa wingi huamshwa na giza. Wakati usiku(giza) homoni hii huzalishwa kwa wingi na kumfanya mtu apate usingizi. Mwanga wa jua unapoanza kutokeza wakati wa asubuhi uzalishaji hupungua na hivyo kumfanya mtu aamke. Kiasi cha Melatonin wakati wa usiku huwa mara 10 zaidi kuliko mchana

Homoni ya melatonin inapozalishwa huachiliwa kwenye mkondo wa damu kisha kusafirishwa kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Ni watu gani wenye hatari ya kuwa na kiasi cha chini ya homoni ya melatonin?

Kiasi cha homoni hii huwa kwa kiasi kidogo kwa wazee kuliko vijana


Nini huweza kuathiri uzalishaji wa homoni ya melatonini wakati wa usiku?

Uzalishaji wa homoni ya melatonin huathiriwa na mwanga wa taa simu na kompyuta.



Ni jinsi gani uzalishaji wa homoni ya melatonin;

Uzalishaji wa homoni ya melatonin huthibitiwa na sehemu ya ubongo inayoitwa suprakayasmatiki nyuklia. Suprakayasmatiki nyuklia huchochea tezi ya pino kuzalisha kwa wingi na wakati wa mchana kupunguza uzalishaji.

Upungufu kiasi au kuzidi kiasi kwa homoni ya melatonin hauhusiani kupata matatizo yeyote ya kiafya kulingana na tafiti za kisayansi. Hata hivyo matumizi ya dawa za melatonin kwa wingi huweza kupelekea kushuka kwa joto la mwili na kuathiri mfumo wa uzazi.

Dawa za homoni ya melatonin zinapatikana katika mfumo wa tembe, hutumika watu haswa wazee waliovurugika mzunguko wa kulala na kuamka.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

17 Aprili 2020, 08:31:05

Rejea za mada hii;

bottom of page