Imeandikwa na daktari wa ULYclinic
Jumanne, 5 Mei 2020
Norepinephrine
Utangulizi
Norepinephrine ni homoni inayojulikana kwa jina jingine la noradrenaline, homoni hii hufanya kazi kama homoni na nyurotransmita (mjumbe) wa kusafirisha taarifa za mfumo wa fahamu kati ya neva moja na nyingine.Homoni hii hufanya kazi kubwa katika kurekebisha hali ya moyo wa mtu na kumfanya mtu kuwa makini. Hata hivyo pia hufanya kazi kwa kushirikiana na homoni zingine ili kuweza kuthibiti msongo wa mawazo na mazoezi
Huzalishwa wapi?
Norepinephrine huzalishwa na tezi ya adreno medulla sehemu ya ndani ya katika sehemu ya ndani. Sehemu hii ya ndani pia huzalisha homoni inayoitwa adrenaline au kwa jina jingine la epinephrine
Norepinephrine ni homoni iliyo kwenye familia ya homoni za katekolamaini ambazo hujumuisha;
• Epinephrine (adrenaline)
• Dopamine
Kazi za Norepinephrine
• Husaidia moyo kusukuma damu na kuongeza mapigo ya moyo
• Huongeza shinikizo la damu
• Husaidia kuvunjwa vunjwa kwa Mafuta mwilini
• Huongeza sukari mwilini na kusaidia mtu kuwa na nguvu zaidi
• Katika ubongo huthibiti mzunguko wa usingizi, husaidia kuamka , huongeza umakini wa kufanya kazi na utunzwaji wa kumbukumbu
• Hutumika katika kuthibiti hisia
• Katika mazingira ya kutisha homoni hii hutumika pia kumpa ujasiri mtu wa kupambana au kukimbia
• Hutumika kuongeza shinikizo damu endapo litashuka kwa sababu ya dawa.
Kiwango cha homoni ya norepinephrine kinapokuwa kidogo kwenye damu hupelekea hali ya;
• Huzuni
• Woga
• Wasiwasi msongo wa mawazo
• Kuishiwa nguvu
• Kukosa umakini
Kiwango cha homoni ya norepinephrine kinapozidi wkenye damu hupelekea hali ya kuwa na;
• Furaha sana
• Kutaharuki
• Kuongezeka kwa shinikizo la damu
Jinsi gani ya kuweza kuongeza kiasi cha homoni ya norepinephrine mwilini :
• Kufanya Mazoezi
• Kulala usingizi wa kutosha
• Kusikiliza miziki
• Kupenda
• Kutafakari
• Kula vyakula vyenye dopamine kwa wingi ama mfano chocolate
Homoni hii inaweza kutumiwa kama dawa kutibu shoku ya septiki
Baadhi ya dawa ambazo huweza kuongeza kiasi cha dawa za homoniya norepinephrine ni;
• Dawa jamii ya SRIs mfano Cymbalta (duloxetine) na Savella (milnacipran)
• Dawa jamii ya amphetamines mfano dextroamphetamine na Ritalin (methylphenidate)
• Rhodiola rosea, L-carnitine, L-tyrosine and L-theanine
ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
5 Mei 2020, 18:23:27
Rejea za mada hii;
- 1.Britannica.Norepinephrine.https://www.britannica.com/science/norepinephrine. Imechukuliwa 14/4/2020
2.Hormone.Norepinephrine.https://www.hormone.org/your-health-and-hormones/glands-and-hormones-a-to-z/hormones/norepinephrine. Imechukuliwa 14/4/2020
3.EveryDayHealth.Norepinephrine.https://www.everydayhealth.com/norepinephrine/guide/. Imechukuliwa 14/4/2020
4.VeryWellHealth.Norepinephrine.https://www.verywellhealth.com/norepinephrine-what-does-or-doesnt-it-do-for-you-3967568. Imechukuliwa 14/4/2020