Imeandikwa na daktari wa ULYclinic
Alhamisi, 9 Aprili 2020
Progesterone
Utangulizi
Ni homoni jamii ya steroidi inayotolewa na tezi ya Kopazi luteamu, Kopazi luteamu ni tezi muhimu ya mpito inayotengenezwa kwenye ovari ili kutoa homoni ya progesterone katika kipindi cha ovulesheni na mwanzoni mwa ujauzito.
Sehemu zinazozalisha homoni ya Progesterone mwilini:
• Kopasi Luteamu (huzalisha kwa kiasi kikubwa)
• Ovari huzalisha kwa kiasi kidogo
• Tezi za adreno
• Wakati wa ujauzito huzalisha na kondo la nyuma (plasenta)
Jinsi inavyozalishwa na kufanya kazi
Wakati wa mzunguko wa hedhi, yai linapotolewa na ovary(ovulesheni) karibia katika siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, mabaki ya kuta zilizokuwa zimefunika yai , hutengeneza tezi ya Kopasi Luteamu
Kopasi Luteamu huweza kutengeneza homoni ya progesterone na kiasi kidogo cha homoni ya oestridiol
Homoni ya Progesterone huanza kuandaa mwili kwa ajili ya kubeba mimba endapo yai litarutubishwa.
Na endapo yai halitarutubishwa, tezi ya Kopasi Luteamu huanza kuvunjika na uzalishwaji wa progesterone hupungua na mzunguko wa hedhi huanza upya.
Endapo yai litarutubishwa ,homoni ya Progesterone huchochea ukuaji wa ukuta wa mimba ili kupokea yai linalokuja kujipandikiza kwenye mji wa mimba.
Na huanza kuchochea tezi zilizopo kwenye ukuta wa uzazi kutoa virutubisho vya kulea kijusi.
Wakati wa hatua za kwanza za mimba homoni ya Progesterone bado inakuwa inazalishwa na Kopasi Luteamu na Kuendelea kuiwezesha itengeneze plasenta.
Plasenta inapotengenezwa huanza kuzalisha homoni ya progesterone katika wiki ya 8 hadi ya 12 Ya mimba
Wakati wa ujauzito progesterone hufanya kazi za :
• Kukuza kijusi
• Kuchochea ukuaji wa tezi za matiti
• Kuzuia maziwa kutoka
• Na kuimarisha misuli ya nyonga kwa ajili ya maandalizi ya leba
Kiasi cha progesterone hubakia kuwa juu mpaka mama anapojifungua
Jinsi ambavyo Progesterone huthibitiwa:
Utengenezwaji wa Kopasi Luteamu huchochewa na homoni ya lutenazing ambayo huzalishwa sehemu ya mbele ya tezi ya pituitari.
Hii hutokea siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi ambapo yai la kike hutolewa kwenye ovari.
Kopasi Luteamu huanza kuzalisha homoni ya progesterone.
Uzalishwaji wa Progesterone unaposhuka chini hupelekea ukuta wa ndani ya uzazi kuvunjika na kutoka nje kama damu ya mwezi. Hii hutokea endapo yai halijachavushwa na mbegu za kiume.
Kiwango cha homoni kuzidi kwenye damu
Hakuna shida inayotokea kutokana na kupanda kwa kiwano cha homoni hii kwa mama wakati wa ujauzito, lakini hali hii huweza kuambatana na haipaplesia ya adreno kwa mtoto akiwa tumboni na saratani ya matiti hapo baadae.
Kiwango cha homoni kuwa chini kwenye damu
Uchache wa homoni hii huweza kupelekea kukosa hedhi, au kutokuwa na mzunguko sawa, hedhi ndogo au nzito
Na endapo itakuwa ni ndogo katika ujauzito huweza kupelekea mimba kutoka (miscarriage) na Labour ya karibu
Mama anayekaribia kuanza labor huweza kupewa Progesterone ya kutengenezwa
Kazi zingine za progesterone
Huweza kutumika peke ake au kwa muunganiko wa estrogen katika kuweza kutumika kama njia ya uzazi wa mpango kuzuia yai kutolewa
Hutumika pia kama homoni ya ziada wakati wa menopause (hedhi inapokoma) kupunguza dalili za hali hii
ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
9 Aprili 2020 11:45:32
Rejea za mada hii;
- 1.YourHormoneProgesteronehttps://www.yourhormones.info/hormones/progesterone/. Imechukuliwa 8.04.2020
2.LowProgesteroneHealthLinehttps://www.healthline.com/health/womens-health/low-progesterone. Imechukuliwa 8.04.2020
3.WebMdProgesteronehttps://www.webmd.com/vitamins/ai/ingredientmono-760/progesterone. Imechukuliwa 8.04.2020
4.MedicalNewTodayProgesteronehttps://www.medicalnewstoday.com/articles/277737. Imechukuliwa 8.04.2020
5.MedicalNewToday corpus luteam. https://www.medicalnewstoday.com/articles/320433. Imechukuliwa 8.04.2020
6.NCBI. Form and function of the corpus luteum during the human menstrual cyclehttps://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2882116/. Imechukuliwa 8.04.2020