Imeandikwa na daktari wa ULYclinic
Jumanne, 5 Mei 2020
Serotonin
Serotonin
Ni homoni inayofanya kazi nyingi sana mwili , homoni hii hujulikana kama homoni ya utulivu kwa sababu homoni hii huweza kuchochea mtu kuwa na utulivu.
Jina lake la kisayansi ni 5-hydroxytryptamine au 5-HT
Mambo muhimu kuhusu homoni ya serotonin
• Hufanya kazi kama homoni na kama mjumbe(nyurotransimita) wa taarifa
• Husafirisha ujumbe kati ya seli moja ya neva na nyingine
• Serotonin huzalishwa katika utumbo, ubongo, mfumo wa neva na chembechembe sahani za damu
• Serotonin hutengenezwa kwa mabadiliko ya kikemikali ambayo huunganisha protini ya tryptophan na tryptophan hydroxylase kwa ajili ya kuitengeneza
Kazi zake za serotonin
• Kama mjumbe, huweza kuunganisha taarifa kutoka mshipa wa neva moja hadi mwingine
• Huimarisha ufanyaji kazi mzuri wa mfumo wa umeng’enyaji wa chakula
• Huweza kuthibiti hali ya moyo wa mtu kama wasiwasi ,woga na utulivu
• Hutolewa na chembechembe sahani za damu kwa ajili ya kusaidia kugandisha damu kama jeraha limetokea.
• Husaidia mtu kujisikia kichefuchefu pale anapokula kitu cha sumu na utumbo hutoa kwa wingi serotonin na kumsababishia mtu hali hii kwa kuchochea sehemu ya ubongo ya kichefuchefu
• Huimarisha uwezo wa mtu kulala
• Huimarisha uwezo mzuri wa kumbukumbu
Dalili za mtu mwenye kiasi kidogo cha serotonin;
• Kupungukiwa kumbukumbu
• Hali ya moyo wa huzuni
• Kupenda vyakula vitamu au vya wanga
• Kushindwa kulala kirahisi
• Woga na hali ya wasiwasi
Kuwa na kiasi kidogo cha serotonin huweza kupelekea hali ya huzuni
Pia kiasi cha serotonin kikizidi kwenye damu huweza kupelekea mtu kukosa hamu ya tendo la ndoa
Watu wenye upungufu wa homoni hii huweza kupewa dawa za mbadala za kuongeza serotonin kwenye damu.
Dawa zifuatazo huzuia ufanyaji kazi wa homoni ya serotonin;
• Citalopram (Celexa)
• Escitalopram (Lexapro)
• Fluoxetine (Prozac)
• Paroxetine (Paxil, Pexeva)
• Sertraline (Zoloft)
ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
5 Mei 2020, 18:42:07
Rejea za mada hii;
- 1.Medical New Today.Serotonin https://www.medicalnewstoday.com/articles/232248. Imechukuliwa 12/4/2020
2.HEALTH LINE.SEROTONIN https://www.healthline.com/health/mental-health/serotonin . Imechukuliwa 12/4/2020
3.Web Md.Serotonin https://www.webmd.com/depression/features/serotonin. Imechukuliwa 12/4/2020
4.Mayo Clinic.serotonin syndrome https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/serotonin-syndrome/symptoms-causes/syc-20354758. Imechukuliwa 12/4/2020