top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Jumatano, 8 Aprili 2020

Testosterone

Testosterone

Utangulizi

Ni homoni ya androjeni inayosimamia uzalishaji wa shahawa, uimara na ujazo wa misuli na mifupa, uchakatuaji wa Mafuta na uzalishaji wa chembe nyekundu za damu. Testosterone ina wajibu wa kumpa mwanaume sifa zake za kijinsia.

Homoni hii huzalishwa kwa kiwango kikubwa kwa wanaume kuliko kwa wanawake, kwa wanaume huzalishwa kwenye korodani katika seli zinazoitwa Leydig na kwa wanawake huzalishwa na ovari. Kiasi kikubwa cha homoni ya testosterone kinachozalishwa kwa wanawake hubadilishwa na kuwa homoni ya kike oestradiol. Kiasi kidogo pia kianweza kuzalishwa na tezi ya adreno.

Jinsi inavyozalishwa;

Tudhibiti wa uzalishaji wa homoni ya testosterone huongozwa kwa kiasi kikubwa na tezi ya hypothalamus pamojana pituitari. Kwa kawaida homoni ya testosterone huwa kwa kiasi kikubwa wakati wa asuubuh na kupungua jinsi muda unavyokwenda. Tezi ya haipothalamus huzalisha homoni ya GRH, homoni hii huingia sehemu yambele ya pituitary na kuiagiza itoe homoni ya luteinising, homoni hii nayo husafiri kwenye damu na kwenda kwenye tezi za gonads na kuziagiza zitoe homoni ya testosterone. Kiwango cha homoni kinapokuwa juu tezi ya hypothalamus hupunguza uzalishaji wa Homoni ya GRH hivyo maagizo ya uzalishaji yanapungua na kiwango cha uzalishaji hupungua.

Kazi za homoni ya testosterone:

Kazi za ki anabolic- hizi huhusika na utengenezwaji au utunzwaji wa nguvu kwa wanaume:
• Kuipa misuli ujazo na uimara wake
• Kuongeza ukubwa wa mifupa na uimara wake
• Kusaidia ukuaji wa mifupa
• Husaidia kuhifadhi Mafuta sehemu maalumu kwa mwanaume
• Husaidia uzalishaji wa chembechembe nyekundu za damu

Kazi za ki androgeniki- hizi huhusika na shughuli za kubarehe;

• Kukua kwa ogani za uzalianaji kama uume
• Kutengenezwa kwa shahawa
• Kumfanya mwanaume awe na Sauti kubwa (besi)
• Huotesha ndevu na nywele sehemu za siri na kwenye kwapa
• Hukuza koromeo
• Kupanua Kifua na mabega
• Huongeza kuzalishwa kwa Mafuta kwenye ngozi na tezi za jasho
• Husaidia katika kuchochea hisia za mapenzi
• Husaidia katika ukuaji wa shahawa

Dalili za kiwango kidogo cha homoni kwenye damu;

• Kushindwa kusimamisha uume
• Kupunguzwa kwa hisia za mapenzi
• Uzalishwaji mdogo wa shahawa
• Kuota chuchu kwa wanaume

Upungufu wa muda mrefu wa homoni hii huweza kupelekea
• Kukosa nywele za kiume(ndevu, nywele sehemu za siri)
• Kuwa na ujazo mdogo wa misuri
• Kukosa nguvu za kiume
• Kuongezeka kwa mafuta mwilini

Upungufu wa homoni ya testosterone huweza kupelekea mifupa kuwa dhaifu na kuvunjika kirahisi, hali ya moyo kubadilika na kuishiwa nguvu na kusinyaa kwa pumbu.


Sababu ambazo zinaweza kupelekea homoni hii kushuka :

• Majeraha kwenye pumbu
• Kupata Maambukizi kwenye pumbu
• Matumizi ya baadhi ya dawa
• Magonjwa yanayoharibu mfumo wa homoni kama kisukari,magonjwa ya figo na ini ,uzito kupita kiasi (obesity) pamoja na HIV

Dalili za kuzidi kwa homoni ya Testosterone;

Kwa mwanamke hupata hedhi isiyo na mpangilio, na isitoshe kutoona hedhi kwa muda Fulani. Hata hivyo pia husababisha mwanamke kuwa na sifa kama za mwanaume mfano kuwa na sauti nzito na besi, kisimi kuwa kikubwa kama uume ,matiti madogo, chunusi nyingi kuota ndevu.

Uzalishaji wa homoni hupungua kwa jinsi umri wa mtu unavyokwenda.

Kuanzia umri wa miaka 40 na Kuendelea kiasi cha homoni huanza kushuka kwa asilimia 1.6 kila mwaka kulingana na tafiti zilizofanywa


Kiasi cha wingi wa testosterone huweza kupimwa kwenye damu. Zipo dawa mbadala za kutumia ili kurekebisha upungufu wa homoni hii.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

8 Aprili 2020 20:40:14

Rejea za mada hii;

bottom of page