Kurasa hii imeorodhesha homon mbalimbali zinazopatikana kwenye mwili wa binadamu
Estradiol
Oestradayo (Estradiol) ni homoni yenye nguvu Zaidi na umuhimu katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanamme. Homoni ya estradiol hujulikana pia kama Oestradiol au E2 ni moja ya homoni kati ya homoni nne aina ya Estrogen ambazo zingine ni Estrone na Estriol na estetro.
Somatostatini ni homoni inayozalishwa karibia katika kila ogani ndani ya mwili, hata hivyo seli nyingi zinazozalisha homoni hii hupatikana kwenye mfumo wa gastrointestino na mfumo wa neva.
Homoni ya glukagoni inayofayofanana na peptaidi (Glucagon like peptide 1) ni homoni inayozalishwa kwenye mfumo wa gastrointestino kufuatia mwitikio wa chakula kinacho ingia tumboni, hujulikana kwa jina jingine la incretin.