Huduma ya kwanza
Huduma ya kwanza ni nini?
Huduma ya kwanza ni matunzo au msaada wa awali anaopatiwa mwathirika wa janga kabla ya mtaalamu wa afya kuwasili eneo la tukio. Matunzo hayo hulenga kuzuia madhara makubwa yanayoweza kujitokeza, kuokoa maisha au kuharakisha uponyaji kutokea.
Mtu wa umri wowote ule anapaswa kujifunza na kufahamu kuhusu namna ya kutoa huduma ya kwanza ili kuweza kukabiliana na dharura/majanga yanayoweza kujitokeza. Katika sehemu hii utajifunza namna ya kutoa huduma ya kwanza kwenye majanga mbalimbali.
Majukumu yako kama mtoa huduma ya kwanza
Kwenye dharura, kazi yako kuu ni kutoa huduma sahihi na kwa wakati inayotakiwa kwa mgonjwa kabla ya kuwasili kwa wataalamu wa afya katika eneo la tukio. Hata hivyo utakuwa na kazi zingine za kiongozi ili kuweza kukabiliana na hali iliyojitokeza kwa ufanisi Zaidi. Mfano endapo tukio la dharura limetokea kabla ya kuwasili kwa mtaalamu wa afya¸ wewe kama mtoa huduma ya kwanza utatakiwa kuwaongoza watu walio pembeni yako ili kumsaidia mhanga wa tukio. Utatakiwa kumpa madaraka mtu mmoja kugandamiza mshipa wa damu unaovuja, mwingine kuleta kile na mwingine kufanya kile. Hakikisha unatuliza akili na fanya kazi kwa utulivu wakati huo ukitumia watu walipo kukusaidia kwa kuwapa maelekezo sahihi, kwa wakati sahihi na kwa lugha nzuri.
Wakati unaenndelea kutoa huduma ya kwanza, hakikisha unaandika nini ambacho umekifanya kwa rejea ya hapo baadae na pia kuwakabidhi wataalamu wa afya kwa maandishi nini ulichokifanya kwa mhanga wa tukio.
Kumbuka kuwa unatakiwa kuchukua tahadhari za kiafya kujikinga dhidi ya hatari ya kupata maambukizi au jeraha wakati unatoa huduma ya kwanza kwa kufuata miongozo ya kuzuia na kudhibiti maambukizi kwa kitiba infection prevention and control- IPC.
Majukumu ya mtoa huduma ya kwanza
Kiufupi, majukumu ya mtoa huduma ya kwanza ni;
-
Kuhakikisha usalama wako na wale unaowaagiza
-
Kudhibiti tukio kwa mujibu wa taratibu zinazotakiwa
-
Kupiga simu kwa wataalamu wa afya au mtoa huuma za dharura kwa wakati unaotakiwa
-
Kugawa majukumu kwa watu wanaokuzunguka
-
Kumpatia mhanga wa tukio huduma ya kwanza iliyo sahihi na kwa wakati
-
Kuandika taarifa ya nini ulichokifanya kwa ajli ya kuipatia timu ya huduma za dharura itakapowasili
-
Kufanya makabidhiano ya mgonjwa na na taarifa muhimu kwa mtaalamu wa huduma za dharura atakapowasili
Hali na mazingira hatari wakati wa kutoa huduma ya kwanza
Mazingira yafuatayo ni hatari wakati wa kutoa huduma ya kwanza
-
Sehemu yenye magari yanayoenda kwa mwendo kasi
-
Barabara inayoteleza
-
Eneo lenye joto kali
-
Kina kirefu cha maji au maji yanayoenda kwa kasi kubwa
-
Kwenye kifaa chenye umeme au waya ambayo upo wazi
-
Mgonjwa aliyekunywa pombe au kutumia dawa za kulevya
-
Sehemu yenye watu wengi
-
Mazingira yenye sumu (kwenye hewa n.k)
-
Sehemu yenye damu na majimaji ya mwili wa mhanga
Endapo upo kwenye mazingira haya hakikisha usalama wako kwanza kabla ya kutoa huduma kwa kuvaa vifaa kinga na kumweka majeruhi sehemu salama. Unapomhamisha majeruhi, hakikisha unazingatia kanuni za kuhamisha majeruhi ili kuepuka jeruhi shingo na uti wa mgongo.
Kusoma makala hii ama kufahamu kuhusu kutoa huduma ya kwanza hakukupi dhamana ya kufanya huduma ya kwanza mwenyewe, siku zote unatakiwa uwapigie wataalamu wa afya kwa ajili ya msaada zaidi, kwa huduma za dharura tafadhari piga simu namba 112 (kwa Tanzania).
Chagua aina ya janga hapo chini kusoma zaidi. Endapo hujapata unachokitafuta, andika unachotaka kwenye boksi juu ya tovuti hii kilichoandikwa 'Tafuta chochote hapa...' na endapo hujapata kabisa wasiliana na daktari wako au daktari wa ULY CLINIC kupitia namba za simu chini ya tovuti hii kwa msaada zaidi.
Chagua mada kusoma kuhusu namna ya kutoa huduma ya kwanza
Bofya hapa kwenda kwenye kurasa kuu yenye orodha ya huduma ya kwanza au kwa kubonyeza baadhi ya zilizoorodheshwa hapa chini. Unaweza tumia pia boksi la 'Tafuta chochote hapa...' hapa juu ya tovuti hii kusoma kuhusu huduma ya kwanza ambayo unaitafuta lakini itakupasa kuandika neno na huduma ya kwanza unayoitaka mfano 'kushuka kwa sukari-huduma ya kwanza'. kisha bofya tafuta
-
Kupaliwa
-
Namna ya kufanya CPR
-
Aliyevunjika
-
Kung'atwa nyoka
-
Kuungua
-
Aliyezama maji
-
Kupigwa shoti
-
Shambulio la moyo
-
Kudhuriwa na sumu
-
Bruizi (kuvilia kwa damu)
-
Mdudu sikioni
-
Kushusha homa
-
Kufungua njia ya hewa
-
Kutambua dalili za homa ya uti wa mgongo
-
Kutambua dalili hatari za kiharusi
-
Kutambua dalili hatari za mshituko wa moyo
-
Huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali
-
Mshiko wa asthma(pumu ya kifua)
-
Mtu mwenye hofu na kupumua haraka haraka(panic attack)
Makala nyingine muhimu kwenye utoaji wa huduma ya kwanza, bofya kusoma
-
Namna ya kupima viashiria uhai (joto, mapigo ya moyo, presha na mapigo ya upumuaji)
ULY CLINIC inakukumbusha uwasiliane na daktari wako siku zote mara utakapopatwa na shida inayohitaji huduma wa kwanza wakati ukichukua hatua ya kukabiliana nayo
Ukiwa Arusha sasa unaweza kupata Huduma ya kwanza kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii