top of page

Huduma ya kwanza

Katika sehemu hii utajifunza kuhusu huduma ya kwanza kwenye matukio mbalimbali ili uweze kuwa msaada pale itakapohitajika kabla wataalamu wa afya hawajafika kwenye tukio

Huduma ya kwanza- Mtu mwenye maumivu ya chembe ya moyo

Huduma ya kwanza- Mtu mwenye maumivu ya chembe ya moyo

Huduma ya kwanza kwa maumivu ya chembe ya moyo ni kumpumzisha mgonjwa, kumpa maji kidogo, na kuepuka kumpa chakula kizito au dawa za maumivu. Ikiwa maumivu ni makali au yanaambatana na dalili hatarishi, mpeleke hospitali mara moja.

Maumivu ya koo huduma ya kwanza

Maumivu ya koo huduma ya kwanza

Kusukutua kwa maji yenye chumvu au magadi, kupumzisha koo, kulala muda wa kutosha na kuongeza unyevu kwenye koo ni baadhi ya mbinu za kupunguza maumivu ya koo.

Kutapika safarini

Kutapika safarini

Kutapika wakati wa kusafiri ni sindromu inayotokea mtu anapokuwa kwenye mwendo aina Fulani na mara nyingi huisha mara mwendo unaisha na hutokea sana wakati wa kusafiri.

Kumwagikiwa na kemikali machoni- Huduma ya kwanza

Kumwagikiwa na kemikali machoni- Huduma ya kwanza

Kumwagikiwa na kemikali kwenye macho inapaswa kuchukuliwa kama tukio la kupata matibabu ya dharura na endapo hatua zisipochukuliwa mapema, inaweza pelekea kuharibika kwa umbo la jicho/macho, matatizo ya uono, ukavu, presha na hata upofu wa macho. Ukubwa wa jeraha na athari zinazoweza kujitokeza hutegemea aina ya kemikali, kiwango kilichomwagikia na muda wa kemikali kuwa katika jicho/macho.

Kujifungulia nyumbani- Huduma ya kwanza

Kujifungulia nyumbani- Huduma ya kwanza

Kujifungua nyumbani inatafsiriwa kuwa ni kujifungua eneo lolote nje ya kituo cha afya, na mama hupatiwa huduma kutoka kwa wakunga wa jadi au ndugu na jamaa. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha kujifungu nyumbani hata hivyo kuna athari pia za kujifungulia nyumbani kama vile vifo kwa wajawazito na vichanga hasa katika nchi zinazoendelea.

bottom of page