top of page
Anafailaksia
Mwandishi:
ULY CLINIC
21 Julai 2021 19:12:31
Anafailaksia ni nini?
Anafilaksia ni mzio mkubwa wa dawa unaotokea dakika chache tu baada ya kutumia dawa au kitu kinachosababisha mzio. Hali hii inahitaji matibabu ya haraka sana ilikuokoa maisha ya muathirika.
Dalili
Dalili za anafailaksia ni;
Kupoteza fahamu
Kuvimba kwa ngozi, kutokwa jasho au kupauka au kupasuka na kutokwa na malengelenge makubwa
Kuhisi joto la ghafla baada ya kutumia dawa
Kuhisi unakabwa na kitu shingoni
Kichefuchefu, kutapika au kuharisha
Maumivu ya tumbo
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Mapigo ya mishipa ya damu kwenda haraka
Kutokwa na kamasi
Kupiga chafya
Kuvimba kwa ulimi na midomo
Imeboreshwa,
6 Juni 2022 15:00:43
bottom of page